The House of Favourite Newspapers

Mapigano Yaibuka Nchini India Kupinga Mfumo Mpya wa Vijana Kujiunga na Jeshi

0
Askari nchini India wakikusanya vijana kwa nguvu kujiunga na jeshi

POLISI Kaskazini mwa India wamelazimika kufyatua risasi kutawanya maandamano ya wananchi ambao walikuwa wanapinga mfumo mpya wa uandikishaji vijana wa kujiunga na Jeshi nchini humo.

 

Mamlaka ya Mji huo iliamua kuzima mtandao wa intaneti kwa muda wa masaa 24 ili kusaidia kusimamisha maandamano hayo.

 

Serikali ya Waziri Mkuu Narendra Modi imetangaza uandikishwaji mpya kwenye jeshi la wanajeshi wenye sialaha milioni 1.38 ikiwa na lengo la kupunguza wastani wa umri pamoja na gharama za malipo ya kustaafu.

 

Kwa mujibu wa ANI washirika wa shirika la habari la Reuters limeripoti kuwa waandamanaji walitupa mawe kwa askari pamoja na Maafisa wa Serikali ili kuzuia zoezi hilo lakini Polisi hawakuwa na namna nyingine zaidi ya kutumia silaha ili kuwatawanya waandamaanaji hao.

 

“Ndiyo tumepiga risasi kadhaa ili kuwatawanya waandamanaji.” Alisema askari mmoja ambaye hakutana jina lake litajwe.

Vijana wameandamana na kuharibu miundombinu ikiwemo mabehewa ya Treni pamoja na Reli

Ingawa hadi sasa hakuna taarifa yoyote ile ya majeruhi.

 

Mfumo upya unaofahamika kwa jina la njia ya moto umetambulishwa nchini humo ambao utaandikisha vijana wa kiume na wa kike wenye umri wa kuanzia miaka 17 na nusu hadi 21 na watahudhuria mafunzo kwa kipindi cha miaka 4 baada ya hapo robo ya kundi hilo ndiyo litakalo ajiriwa na jeshi.

 

Mgomo huo umechagizwa zaidi na hoja ya hatima ya wale watakaorudi nyumbani baada ya miaka hiyo minne, mmoja wa kijana amenukuliwa akisema kuwa baada ya miaka minne akirudi nyumbani atakuwa hana makazi sasa ataishi vipi?

Leave A Reply