Kartra

Makambo Aachana na Horoya

MSHAMBULIAJI Heritier Makambo ameachana na klabu yake ya Horoya inayoshiriki Ligi Kuu nchini Guinea baada ya makubaliano ya pande zote mbili kufanyika.

 

Makambo alisajiliwa na Horoya kwa mkataba wa miaka mitatu na mpaka sasa alikuwa ameitumikia timu hiyo kwa misimu miwili tu.

 

Kuvunjwa kwa mkataba huo ni taarifa nzuri kwa mabosi wa Yanga ambao inaelezwa wamekuwa wanahitaji mchezaji huyo arejee katika kikosi chao.

 

Ilielezwa Yanga walipeleka ombi la kuhitaji kumsajili mchezaji huyo lakini ilishindikana kutokana na mabosi wa Horoya kuhitaji pesa nyingi.

 

Kupitia ukurasa rasmi wa Instagram ya klabu ya Horoya ulimshukuru Makambo kwa kuwa nae kwa misimu miwili mfululizo na kumtakia kila la kheri.

 

“Ahsante (Mercì) kwa misimu miwili tangu ulivyofika, tunakutakia kila la kheri katika kipaji chako,” ilieleza taarifa hiyo.

GOMES Ataja SILAHA za KUIMALIZA YANGA, YANGA Yajibu MAPIGO, | KROSI DONGO…


Toa comment