The House of Favourite Newspapers

Makambo Akerwa na Ngumi Yakotei

Heritier Makambo

HERITIER Makambo amesema kwamba Simba ni timu ya kawaida sana lakini akaongeza kwamba James Kotei alifanya kosa kubwa kumpiga ngumu Gadiel Michael.

 

Hiyo ni ‘dabi’ yake ya kwanza kuicheza Makambo ali­yetua kuichezea timu hiyo kwenye msimu huu wa ligi aki­tokea Motema Pembe.

 

Akizungumza na Championi Jumatano, Makambo alisema Simba siyo wa kuwaho­fia kiviile huku akiitaja presha ya mashabiki ndiyo inasababisha mchezo kuwa mgumu.

 

Mshambuliaji huyo alishindwa kuficha kuchukizwa kwake kwa kiungo mkabaji wa Simba Mghana, Kotei kumpiga ngumi beki wao Gadiel.

 

“Nimejifunza mengi kutokana na mechi hii iliyoikutanisha Simba na Yanga ambazo ndiyo timu kubwa na kongwe hapa nchini, kikubwa presha ya mashabii ndiyo inafanya mchezo kuwa mgumu.

 

“Lakini kingine nimejifunza ni baadhi ya wachezaji kucheza kwa kupania na kusababi­sha kufanya vitendo ambavyo havistahili katika soka ikiwemo kitendo cha mchezaji wa Simba (Kotei) kumpiga ngumi Gadiel.

 

“Siyo kitendo cha kiungwana kiukweli, mashabiki wamekuja uwanjani kuangalia bu­rudani inayotokana na soka safi na siyo ngumi, hivyo binafsi nimewao­na Simba na kujifunza vitu vingi, tutaonana kwenye mzunguko wa pili wa ligi,”alisema Makambo.

Comments are closed.