The House of Favourite Newspapers

Makambo Aletewa Kiatu Maalum Toka Uturuki

Heritier Makambo

MSHAMBULIAJI wa Yanga, Heritier Makambo hivi karibuni anatarajia kupokea kiatu kipya cha kuchezea kutoka nchini Uturuki baada ya kununuliwa na mmoja wa wafuatilia wa soka nchini Tanzania, Mzee Karama.

 

Mdau huyo mwenye duka la mich­ezo la Just Fit lililopo Mlimani City jijini Dar amemnunulia kiatu hicho mshambuliaji huyo sambamba na beki Abdallah Shaibu ‘Ninja’ ambavyo atawapa hivi karibuni kwa ajili ya kuvi­tumia kwenye michezo ya ligi.

 

Mzee Karama ameliambia Cham­pioni Ijumaa, kuwa anamletea Makambo viatu hivyo kwa ajili ya kuongeza idadi ya mabao ambapo tayari ameshavilipia.

 

“Nipo Uturuki na nimenunua viatu vya Makambo na Ninja ambavyo nawaletea, tayari nime­shavilipia. Namletea Mkambo hili ma­bao yaongezeke,” alisema Mzee Karama.

 

Comments are closed.