The House of Favourite Newspapers

Makambo ampiga mkwara Kagere

AKIIONGOZA Yanga leo i takapovaana na Tanzania Prisons ya Mbeya, mshambuliaji wa timu hiyo, Mkongoman, Heritier Makambo, ni kama ameanza nyodo vile baada ya kuwafikia washambuliaji wa Yanga, Emmanuel Okwi na Meddie Kagere kwenye idadi ya mabao ya kufunga.

 

Makambo, juzi Alhami­si alifikisha mabao saba ambayo yamefungwa na Okwi na Kagere wakati Yanga ilipocheza na Polisi Tanzania katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliopigwa Uwanja wa Taifa na ma­tokeo. Yanga ilishinda 3-0.

 

Mkongoman huyo ali­yefunga mabao matatu kwenye mechi tatu mfu­lulizo za ligi za hivi karibuni, anamfukuzia mshambuliaji wa Mbeya City, Eliud Ambokile, anayeongoza katika ufungaji akiwa amaepachika mabao nane. Tofauti ni bao moja tu.

 

Akizungumza na Cham­pioni Jumatatu, Makambo al­isema moja ya malengo yake aliyoyapanga ni kuona anaen­delea na kasi yake ya kufunga mabao katika michezo inayo­fuata ya ligi.

Makambo alisema, kasi yake ya kufunga mabao im­erejea baada ya kuyafanyia kazi makosa yaliyokuwa yanamsababisha ashindwe kupachika mabao huku akifua­ta maelekezo ya kocha wake, Mwinyi Zahera kabla na baada ya mechi.

 

“Nimejifunza vitu vingi kwa kipindi kifupi nilichokuwa Yanga, kwa kifupi mashabiki wanapenda kuona timu yao ikipata matokeo mazuri am­bayo siyo ya kufungwa, wao wanapenda ushindi tu.

 

“Katika mechi za hivi kar­ibuni kabla ya kwenda Shin­yanga kucheza Mwadui FC, mashabiki walikuwa wanabeza kiwango changu kwa kuanza kuniongelea vibaya, lakini nashukuru maneno hayo hay­a kunitoa mchezoni zaidi nil­i ongeza bidii ya mazoezi na kuongez a umakini ka­tika kufun­ga mabao.

 

“Nikaan­za kufunga mechi na Mwadui na michezo mingine iliyofuat a nikaende­lea kufunga ikiwemo na Kagera Sugar kabla ya kucheza na JKT Tan­zania am­bayo nayo nilifunga, hivyo nimepanga kuendelea na kasi yangu hii ya kufunga mabao,” alisema Makambo.

WILBERT MOLANDI, Dar es Salaam

Comments are closed.