The House of Favourite Newspapers

Makambo: Ukurasa Ndiyo Kwanza Unaanza

0

HERITIER Makambo, nyota wa kikosi cha Yanga, ameweka wazi kuwa ukurasa wake wa mabao ndiyo kwanza
unaanza kufunguliwa kwani
hajachuja katika suala la ufungaji, akitamba kwamba akipewa nafasi atafunga.

 

Nyota huyo kwa sasa ni kinara wa utupiaji ndani ya Yanga kwenye Kombe la Shirikisho akiwa ametupia mabao matatu, ilikuwa mbele ya Ihefu FC wakati Yanga iliposhinda mabao 4-0.


Akizungumza
na Championi Jumamosi, mshambuliaji huyo ambaye anapewa nafasi ya kuanza kesho mbele
ya Tanzania
Prisons kutokana na Fiston Mayele kuumia, alisema kuwa kazi bado inaendelea.

 

“Naona wanasema kwamba uwezo unakuwa umeshuka kwa kuwa sifungi, katika hilo ninasema hapana kwa sababu ili ufunge inabidi uwe unapata nafasi na pia nimekuwa nikifanya mazoezi kila siku jambo ambalo linalinda
uwezo wangu.


“Ninachoweza
kusema ni kwamba wasubiri, kazi bado inaendelea na kwa namna ambavyo mashabiki wamekuwapamoja nasi kila muda waendelee na moyo huo, sisi tutazidi kupambana kwa ajili
ya kupata matokeo,” alisema
Makambo.

STORI: LUNYAMADZO MLYUKA, Dar es Salaam

Leave A Reply