The House of Favourite Newspapers

MAKAMPUNI 500 KUSHIRIKI MAONYESHO YA PILI YA BIDHAA DAR

0
Waziri Mwijage akizungumza na wanahabari.

ZAIDI ya Makampuni 500 yanatarajia kushiriki katika maonesho ya pili ya bidhaa za viwanda  yanayotarajia kufanyika Desemba 7 hadi hadi 11, mwaka huu katika Viwanja vya Maonesho vya Mwalimu  Nyerere (sabasaba) jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage, amesema katika maonyesho ya mwaka jana makampuni 472 pekee ndiyo yaliyoshiriki.

“Lengo kuu la maonesho haya ni kujenga jukwaa kwa wadau wa viwanda kupata fursa ya kujadiliana, kubadilisha uzoefu na kutangaza biashara za watanzania wote wanaomiliki viwanda vidogo, vya kati na vikubwa,” amesema Mwijage.

NA DENIS MTIMA/GPL

Matukio kama haya na mengine, Install App Yako ya Kijanja na Namba Moja Tanzania ya Global Publishers

Android ===>Google Play

iOS ===>Apple Store

VIDEO: Dk Shika Atamba Kutikisha Usiku wa 900 Itapendezaa

Leave A Reply