The House of Favourite Newspapers

Makamu wa Rais Acacia, Mwanyika na Lugendo Watiwa Mbaroni

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) imewakamata aliyekuwa Makamu wa Rais wa Kampuni ya Uchimbaji Madini ya Acacia, Deo Mwanyika na Mshauri wa Serikali ndani ya kampuni hiyo, Alex Lugendo.

Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Brigedia Jenerali John Mbungo, alisema wanawashikilia watu hao tangu juzi na kwamba leo wanaweza kufikisha mahakamani kufunguiwa mashtaka kwa tuhuma zinazowakabili.

 

“Mwanyika na Alex tuliwakamata kwa tuhuma za matumizi mabaya ya ofisi katika nyanja ya madini. Wakiwa viongozi waandamizi walishindwa kusimamia nchi ipate mapato kama ilivyotakiwa kwa mujibu wa sheria,” alisema Mbungo.

 

Deo Mwanyika alijiunga na Acacia mwaka 2001 akiwa ameitumikia kwa miaka 17 ambapo alitangazwa kujiuzulu Agosti 24 mwaka huu kwa barua ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa Acacia, Peter Galeta kwenda kwa wafanyakazi wote wa kampuni hiyo.

Comments are closed.