Makamu Wa Rais Ashiriki Kumbukizi Ya Hayati Abeid Amani Karume – Picha
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk. Hussein Ali Mwinyi ameongoza kisomo cha Dua na Hitma ya kumuombea Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Hayati Sheikh Abeid Amani Karume, iliyofanyika Afisi Kuu CCM Kisiwandui Zanzibar tarehe 07 Aprili 2024.
Viongozi mbalimbali wameshiriki akiwemo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango.