The House of Favourite Newspapers

Rais Samia Ashiriki Maadhimisho ya Miaka 30 tangu kutokea Mauaji ya Kimbari Kigali, Rwanda

0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Samia Suluhu Hassan akitoa Heshima mara baada ya kuweka shada la maua kwenye eneo la Makaburi ya kumbukumbu ya mauaji ya Kimbari Kigali nchini Rwanda tarehe 07 Aprili, 2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan leo Aprili 7, 2024 ameshiriki Maadhimisho ya Miaka 30 tangu kutokea Mauaji ya Kimbari Kigali nchini Rwanda

Maadhimisho hayo ya miaka 30 yamehudhuriwa na viongozi kutoka nchi mbalimbali.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa pamoja na viongozi mbalimbali wakimshuhudia Rais wa Rwanda Mhe. Paul Kagame akiwasha mwenge wakati wa kumbukumbu ya mauaji ya Kimbari Kigali nchini Rwanda tarehe 07 Aprili, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa pamoja na viongozi mbalimbali kabla ya kushuhudia kuwashwa kwa mwenge wakati wa kumbukumbu ya mauaji ya Kimbari Kigali nchini Rwanda tarehe 07 Aprili, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa pamoja na viongozi mbalimbali mara baada ya kuweka shada la maua kwenye eneo la Makaburi ya kumbukumbu ya mauaji ya Kimbari Kigali nchini Rwanda tarehe 07 Aprili, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akielekea kwenye eneo la Makaburi kwa ajili ya kuweka shada la maua wakati wa Maadhimisho ya miaka 30 tangu kutokea mauaji ya Kimbari Kigali nchini Rwanda. Maadhimisho hayo ya miaka 30 yamefanyika katika Makumbusho ya Mauaji ya Kimbari, Kigali nchini Rwanda na kuhudhuriwa na viongozi kutoka nchi mbalimbali tarehe 07 Aprili, 2024.

Leave A Reply