The House of Favourite Newspapers

Makamu Wa Rais Dkt, Mpango Azindua Kongamano La Biashara Kati Ya Tanzania Na Umoja Wa Ulaya

0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango akizindua kongamano hilo.

Februari 23, 2023, DAR ES SALAAM:Kongamano la Biashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na Nchi za Umoja wa Ulaya linalofanyika kuanzia leo tarehe 23 hadi 24 Februari, 2023  limefunguliwa rasmi na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Baada ya kusainishana mikataba.

Wakati akifungua Kongamano hilo, Makamu wa Raisamewakaribisha wawekezaji kutoka nchi wananchama wa Umoja wa Ulaya kuja kuwekeza nchini kwenye maeneo yanayoendana na mahitaji ili kuiwezesha Tanzania kutimiza malengo ya Dira ya Taifa  ya 2025 na kukuza kutoka uchumi wa kati wa chini hadi uchumi wa kati wa katikati.

Akianinisha maeneo mbalimbali ambayo wawekezaji hao wanaweza kuwekeza, Dkt. Mpango amesema Tanzania ina fursa nyingi za uwekezaji  ambazo wanaweza kuwekeza ikiwemo kilimo, viwanda vya kuongeza thamani mazao ya kilimo,  viwanda vya dawa na vifaa tiba, ujenzi, sayansi, teknolojia, maendeleo ya viwanda katika kizazi cha nne ( 4) ( 4th IndustrialEvolution).

Aidha, Amesema Serikali ya Awamu ya Sita imedhamiria kuboresha mazingira ya uwekezaji na ufanyaji biashara kwa kuendelea kurekebisha sheria, kuboresha mifumo ya  ulipaji kodi ikiwemo sera za ulipaji kodi kwa nchi kumi, kuimarisha kituo cha uwekezaji Tanzania ( TIC) na Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji Zanzibar (ZIPA),Kuimarisha upatikanaji wa umeme, Uendelezaji wa Bandari ya Dar es salaam, Tanga na Mtwara, Bandari kavu ya kwala, ujenzi wa barabara na reli, na uanzishaji wa Sheria ya Uwekezaji ya 2022 ikifuta ile ya 1997

Aidha, Amesema Serikali imefanya jitihada mbalimbali za kuifungua  nchi kwa uchumi wa dunia kwa kwa lengo ya kuifanya tanzania kuwa kitivo cha biashara na uwekezaji na kupanua biashara   Kujifunza, kubadilishana uzoefu kufahamiana na kutafusa fursa  na kuingia makubaliana  kibiashara.

Vilevile, Wakati wa ufunguzi wa kongamano hilo pia viongozi mbalimbali wa Serikali na Taasisi  kutoka Tanzania wakiwemo Mawaziri wa sekta za uzalishaji akiwemo  waziri wa nchi  Ofisi ya Rais Uchumi, Kazi na Uwekezaji  wa Zanzibar Mhe. Mudrick Soragha ,Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbalawa, Manaibu Waziri, Makatibu Wakuu , Manaibu Makatibu Wakuu, Mabalozi wa Tanzania katika nchi za Umoja wa Ulaya akiwemo Mhe. Balozi  Jestas Abouk Nyaman, Wakuu wa Taasisi za umma na sekta binafsi pamoja na wajumbe wa kamati ya Viwanda, Biashara Kilimo na Uvuvi.

Aidha, Viongozi wa Serikali na Taasisi kutoka na umoja wa Ulaya  wamehudhuria akiwemo  Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania Mhe.  Manfredo Fanti, Mhe. M Waziri wa Mambo ya Nje, Biashara na vivutio vya uchumi  wa Ufaransa Mhe. Mr. Olivier Becht; Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Ulaya huduma za nje Bi Helena Konig na Makamu wa Rais wa Benki ya Uwekezaji ya Umoja wa Ulaya  Mhe.Thomas Östros.

Katika hotuba yake Waziri wa Ufaransa ameainisha  nia ya Ufaransa kuimarisha uwekezaji  Tanzania na Afrika Mashariki na jinsi Serikali yake imekuwa ikishirikiana na Serikali ya Tanzania hususan katika sekta za kimkakati.

Naye Makamu wa Rais wa  benki ya Uwekezaji ya Umoja wa Ulaya (EIB)  amesema  Benki hiyo ya EIB imerudi nchini baada ya UVICO- 19 iko tayari kufanya uwekezaji mkubwa  wenye thamani ya EUR milioni 540 kwa kuwawezesha wawekezaji na wafanyabiashara nchini wakiwemo wananwake , maji, utalii na na kampuni zinazojihusisha  wna uchumi wa Blue. Hii itafanyika kupitia ushirikiano na kifedha kati ya EIB na CRDB, NMB, na KCB  pamoja na makubaliano yaliyofanyika leo kati ya  makampuni ya Umoja wa Ulaya na Tanzania  makampuni ya Tanzania itakayowawezesha kuwekeza na kupanua biashara zao  hususani katika utalii, uvuvi.

Aidha, katika kongamano hilo Hati za makubaliano nne (4) zimetiwa saini ambapo Hati ya Makubaliano ya  Huduma ya Usafiri wa Anga uliotiwa saini na Waziri wa ujenzi na uchukuzi Mhe. Prof Mbalawa na Waziri wa mambo ya nje, biashara na vivutio vya uchumi wa Ufaransa Mhe. Olivier Becht ambapo  makubaliano hayo ytawezesha  kuongeza idadi ya safari za ndege kati ta tanzania na ufaransa ikiwemo safari moja kwa moja kutoka dar es salaam kwenda ufarasa  ifikapo mwezi june 2023 kisiwa cha mayotte ambapo makampuni ya ndege ya tanzania yataruhusiwa kusafiri moja kwa moja hadi kisiwa hichokwanza  Tanzania and French direct Zanzibar to France.

Hati nyingine ya makubaliano iliyotiwa saini ni kati ya bandari ya Antwerp-Bruges International na Mamlaka ya Bandari ya Tanzania ambao utaongeza  usimamizi wa bandari na kuimarisha miundombinu ya bandari ikiwemo bandari kavu na bandari za maziwa na kuiongezea uwezo bandari hiyo  ili kuongeza ufanisi wa bandari ya Tanzania.

Hati ya makubalioano ya tatu ilihusu ujenzi wa Mradi wa uzalishaji wa umeme wa Kakono Hydro Power utakaojengwa Mkoani Kagera uliofadhiliwa na Benki ya Maendelo Afrika chini ya ufadhili wa Umoja wa Ulaya.

Ya nne ni hati ni kati yaKnauf Gypsum Tanzania Limited in Kisemvule, Mkuranga  inayopanga kupanua uzalishaji wa gypsum 6.

Kongamano hilo limejumuisha zaidi ya washiriki 800 kutoka nchi za Umoja wa Ulaya na Tanzania linalenga kuwaunganisha washiriki hao  katika kongamano linalolenga kuonyesha fursa za uwekezaji zilizopo Tanzania na wawekezaji wa Tanzania watapata fursa ya kujadiliana  na wafanyabiashara wenzao wa Umoja wa ulaya katika maeneo ya  kilimo, Nishati Uzalishaji, Ujenzi, usafirishaji na Mawasiliano Mikutano ya majadiliano kati ya serikali na wafanyabiashara.

Leave A Reply