The House of Favourite Newspapers

Makatibu Wakuu wa Tanzania, Afrika Kusini Kujadili Fursa za Kiuchumi

0
Katibu Mkuu, Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Aziz Mlima(Kushoto) akizungumza kwenye mkutano huo.
Baadhi ya makatibu wakuu wa wizara mbalimbali kutoka Tanzania na Afrika kusini wakisikiliza jambo kwenye mkutano.
Baadhi ya makatibu wakiwa kwenye picha ya pamoja.

MAKATIBU wakuu wa wizara mbalimbali Tanzania na wa nchi ya Afrika Kusini leo wamekutana na kujadili mambo mbalimbali yanayohusu masuala ya kibiashara na uchumi.

Akizungumza katika mkutano huo, Katibu Mkuu, Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Aziz Mlima alisema kuwa mkutano huo unalenga hasa kujadili mambo mbalimbali ya masuala ya kiuchumi katika sekta mbalimbali  kuelekea ujio wa Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma anayetarajia kuzuru nchini Mei 10, mwaka huu.
Katika ujio huo, Rais Zuma anatarajiwa kuambatana na baadhi ya wafanyabiashara wakubwa wa nchi hiyo ili kuweza kubadilishana mbinu mbalimbali za kibiashara. Mkutano huo utakuwa wa siku mbili ambapo pia utafuatiwa na mkutano mwingine wa mawaziri wa Tanzania na Afrika ya Kusini.
Na Denis Mtima/GPL

Leave A Reply