The House of Favourite Newspapers

Makonda Aipongeza Muhimbili kwa Hili

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ameipongeza Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa kuendelea kusaidia wahitaji mara baada ya kufanikisha matibabu Ashraf Hamza, ambaye alikuwa na uvimbe usoni mpaka kwenye jicho lake la kulia.

“Sisi wananchi tukija kusalimia wagonjwa wetu hapa Muhimbili tuangalie na wale wanaozunguka ndugu zetu, kwani uponyaji wa ndugu yako unaweza kuwepo kwa kumsaidia yule aliyepo pembeni yake.”

“Ukienda kwa wanasiasa wengi wanapenda kutoa misaada kwa ajili ya kuonekana na wapiga kura, jambo ambalo sisi katika mkoa wetu wa Dar es Salaam tunafanya kwa ajili ya kuwasaidia wahitaji na sio kuonekana,” amesema Makonda.

Comments are closed.