The House of Favourite Newspapers

Makonda aja na Kampeni ya Sukuma Twende

0

1.Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda akizungumza na wanahabri (pichani hawapo).Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda akizungumza na wanahabari (hawapo pichani).

2.Wanahabari wakichukua tukio.Wanahabari wakichukua tukio.

3.DC Makonda akionesha kipeperushi kilichoandikwa ujumbe mfupi wa maneno wa huduma hiyo ya utoaji taarifa kwa njia ya simu.Makonda akionesha kipeperushi kilichoelekeza namna ya kujiunga na huduma hiyo ya utoaji taarifa kwa njia ya simu za mkononi.

4.Makonda akijaribu kuandika ujumbe wa maeneno kutumia simu zake za mkononi kwa kuonesha wanahabari waliohudhuria mkutano huo.Makonda akijaribu kuandika ujumbe wa maeneno kutumia simu zake za mkononi kwa kuonesha wanahabari waliohudhuria mkutano huo.mtima kipeperushi

Kipeperushi chenye maelezo kuhusu kampeni ya Sukuma Twende.

IKIWA sasa ni takribani wiki moja tangua rais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Pombe Magufuli aingie madarakani rasmi akiwa na kauli ya “Hapa Kazi Tu“ huku akitembelea baadhi ya sekta za utumishi wa umma kwa kushtukiza, naye Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda amekuja na  kampeni aliyoipa jina la “Sukuma Twende”.

Akizungumza na wanahabari leo ofisini kwake jijini Dar es Salaam katika uzinduzi wa kampeni hiyo, Makonda amesema lengo ni kuwasaidia wakazi wa Kinondoni kuondokana na matatizo wanayokumbana nayo wanapokuwa wakihitaji huduma kwenye sekta za utumishi wa umma.

Makonda amesema ujumbe huo utawawezesha kufikisha malalamiko yao kwa kutoa taarifa na ushauri kupitia simu zao za mkononi kwa kuandika ujumbe wa maneno kwenye simu ya mkononi moja kwa moja pindi wanapoona watumishi wa sekta za utumishi wa umma wanazembea au hawajali wananchi katika utoaji huduma.

“Kwa kupokea taarifa za wananchi mbalimbali nitatumia dhamana niliyopewa na kuwafikishia wakuu wa idara au sekta husika, lakini pia nina mamlaka ya kuwaonya kwa barua na hata kuwasimamisha kazi, lengo langu ni kuongeza uwajibikaji katika sekta mbalimbali serikalini,’’ alisema Makonda.

Aidha Makonda amesema kampeni hiyo ya imeandaliwa na ofisi yake kwa kushirikiana na Kampuni ya Push Mobile, hivyo wananchi watatuma ujumbe mfupi wa maneno kwa kuandika neno Kinondoni au ‘KN’ wakiacha nafasi ukifuatiwa na ujumbe mfupi wa maneno iwe ushauri au maoni na baada ya hapo utatuma kwenda namba 15404.

Uongozi huo umepanga kufikisha ujumbe watakaoupokea kutoka kwa wananchi ndani ya wiki moja kwa atakaye kuwa amelalmikiwa sana kutokana utendaje wake.

Aidha Makonda ametaja baadhi ya sekta atakazoanza nazo ni Wizara ya Afya kwa maana ya hospitali zote zilizopo Kinondoni, sekta ya ardhi, biashara, mahakama, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na sehemu nyingine.

NA DENIS MTIMA/GPL

Leave A Reply