MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, amewatunuku zawadi mbalimbali yakiwemo magari maofisa wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kutokana na utendaji wao mzuri kwa jeshi hilo na taifa kwa jumla.
Hafla ya utoaji wa tuzo hizo kwa polisi waliofanya vizuri mwaka 2018 imefanyika katika Ukumbi wa Mlimani City, Dar usiku wa kuamkia leo na kuhudhuriwa na vigogo mbalimbali wa polisi na wadau wengine wa ulinzi na usalama.
Hafla hiyo ya kihistoria kwa jeshi la Polisi na watumishi wake, ilifana kiaina huku maafande wawili, Staff Sajenti Beatrice Grayson Mmbaga na Konstebo John Joseph Mutashobya wakiibuka na magari mapya kama zawadi kutokana na utendaji wao mzuri katika kutekeleza majukumu yao.
Katika utunukiwaji wa zawadi hizo wengine walipatiwa zawadi mbalimbali ikiwemo mifuko ya saruji, mabati, pikipiki na nyinginezo.
Mbali na Makonda, wengine waliohudhuria kwenye hafla hiyo ni Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa, makamanda wengine wa jeshi la polisi, maofisa wa jeshi hilo, wasanii wa Bongo Movies na Bongo Fleva na wadau wengine wa ulinzi nchini.
HABARI/ PICHA: RICHARD BUKOS /GPL
Comments are closed.