The House of Favourite Newspapers

Figisu Mazembe kuanzia airport, Simba wazipangua

    Kikosi cha timu ya Simba.

KIKOSI cha Simba kilitarajiwa kuondoka leo alfajiri kwenda Lubumbashi nchini DR Congo kwa ajili ya mechi ya marudiano ya Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya TP Mazembe kwa ndege ya kukodi.

 

 

Hata hivyo, ulinzi ambao timu hiyo imewekewa jijini humo ni mkubwa, hiyo ni baada ya uongozi wa timu hiyo kupitia mashushushu wake uliokuwa umewatanguliza huko kubaini kuwepo kwa mchezo mchafu ambao TP Mazembe imejipanga nao kuanzia watakapotua uwanja wa ndege kwa ajili kuifanyia Simba, lengo ikiwa ni kuwavuruga kisaikolojia kabla ya mchezo.

Kikosi cha timu ya Mazembe.

 

Kutokana hali hiyo inadaiwa kuwa uongozi wa Simba chini ya bilionea wa timu hiyo, Mohammed Dewji ‘Mo’ umelazimika kuweka ulinzi mkali ili kuhakikisha TP Mazembe hawapati nafasi ya kutimiza mipango yao hiyo.

 

Habari za kuaminika kutoka ndani ya Simba ambazo Championi Ijumaa limezipata, zimedai mashushushu walituma taarifa hizo za kuwepo kwa figisufigisu na kuutaka uongozi kuwa makini juu ya hilo.

 

“Kwa hiyo, kutokana na hali hiyo ndiyo maana uongozi ukaamua timu iondoke Ijumaa kwa ndege ya kukodi na itakapofika nchini humo kuanzia uwanja wa ndege itakuwa chini ya ulinzi mkali ambao tayari umeandaliwa ili kuepukana na hujuma ambazo wapinzani wetu wameziandaa,” kilisema chanzo hicho cha habari.

 

Mratibu wa Simba, Abbas Ally, akizungumzia hilo alisema: “Ni kweli uongozi umechukua tahadhari zote na ni matumaini yangu kila kitu kitakuwa sawa.”

Sweetbert lukonge na Said ally, Dar

Comments are closed.