Makonda Amtmbelea Mtoto Hamis, Muhimbili, Amshushia Maombi – Video

MKUU wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, leo Machi 15, 2019 amemtembelea na kumjulia hali mtoto Hamisi ambaye amelazwa katika Hospital ya Taifa ya Muhimbili akisumbuliwa na tatizo la kuvimba miguu yote miwili.

 

Mbali na kumjulia hali RC Makonda amemfanyia maombi mtoto huyo kwa kumkabidhi mikononi mwa Mungu ili aweze kumponya.

 

Mtoto Hamisi alianza kusumbuliwa na tatizo la miguu miaka kadhaa iliyopita ambapo Global Publishers ilifanya kampeni ya kumchangia kwa ajili ya matibabu ambayo yalifanyika nchini India na akarejea nchini.

 

Lakini kwa sasa tatizo hilo limerejea tena na Hamisi amekuwa akiteseka kwa ugonjwa huo. Unaweza kumtumia chochote au kumjulia hali HAMISI kupitia namba hii, 0716963026 (italeta jina la FATUMA LWIGILA ambaye ni dada yake). Mungu akubariki sana!

 

Toa comment