The House of Favourite Newspapers

MAKONDA APOKEA VIFAA VYA MATIBABU KUTOKA KOREA KUSINI

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (katikati) akiangalia vifaa alivyokabidhiwa kama msaada kutoka serikali ya Korea Kusini kupitia shirika la KOICA.
Makonda akipokea vifaa hivyo kutoka kwa Balozi wa Korea Kusini nchini Tanzania, Geum Young.
Makonda akiwa katika picha ya pamoja na  Balozi wa Korea Kusini nchini Tanzania, Geum Young.

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda leo amepokea Vifaa vya matibabu vyenye thamani ya shilingi milioni 100 kutoka serikali ya Korea Kusini kupitia shirika la KOICA.

 

 

Vifaa vilivyotolewa ni pamoja na Digital X-ray 3, Ultrasound 1, Kabati la usalama wa viumbe (safety cabinet) 1, Mashine 3 za kupima mkojo, mashine ya kuwapa joto watoto njiti pamoja na mashine ya utakitshaji.

 

 

Baada ya kupokea vifaa hivyo kutoka kwa Balozi wa Korea kusini, Geum Young Song Makonda amekabidhi vifaa hivyo kwenye vituo vya afya vya Sinza, Mnazi Mmoja na Mbagala ambako kuna uhaba wa vifaa.

 

 

Kabla ya kupokea vifaa hivyo Makonda alifanya mazungumzo na Balozi huyo wa Korea kusini na kuwasilisha ombi la kujengwa kwa Chuo cha kisasa cha mafunzo ya udaktari na uuguzi ambapo Balozi Geum Young amelipokea kwa mikono miwili ombi hilo.

 

 

Makonda pia amemueleza balozi huyo ombi la kujengwa kwa kituo kikubwa cha upimaji wa magonjwa mbalimbali kwa wananchi kwenye eneo moja ambapo pia amelikubali ombi hilo na kumsifu Makonda kwa moyo wake wa kujali wananchi.

 

 

Kwa upande wake Balozi wa Korea Kusini nchini Tanzania, Geum Young  amesema wametoa vifaa hivyo kuunga mkono kazi kubwa inayofanywa na Mkoa wa Dar es Salaam katika uboreshaji wa sekta ya Afya na wataendelea kusaidiana na serikali.

 

Comments are closed.