The House of Favourite Newspapers

Makonda Ashuhudia Mafuriko, Bil 200 Zapelekwa Mto Msimbazi

MKUU wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda jana amefanya ziara ya ukaguzi wa athari za mafuriko ambapo amesema serikali imeanza kukarabati miundombinu iliyoathiriwa na mvua zinazoendelea kunyesha ikiwemo madaraja, barabara, mito na mifereji.

Akizungumza wakati wa ukaguzi huo Makonda, amesema miongoni mwa maeneo yanayoboreshwa na pesa ipo tayari ni mto msimbazi wenye urefu wa kilomita 19 na eneo la Jangwani ambalo maboresho yake yatagharimu zaidi ya shilingi Bilioni 200 ikiwa ni mkopo kutoka Benki ya Dunia.

Aidha, Makonda amesema hadi sasa jumla ya watu wawili wamefariki kutokana na mvua ambapo amewapa pole wananchi waliokumbwa na athari za mafuriko ikiwemo wale ambao mali zao zimeharibiwa na wengine kulazimika kuyahama makazi yao.

Katika hatua nyingie Makonda amewataka wananchi kuchukuwa tahadhari dhidi ya ugonjwa wa Dengue kwa kuhakikisha wanatokomeza mazalia ya mbu na kuhakikisha wanawahi vituo vya afya pindi wanapoona dalili za homa.

Comments are closed.