The House of Favourite Newspapers

Makonda Asimikwa Uchifu Na Wazee Wa Mara

0

Wazee wa Mkoa wa Mara wamemsimika Uchifu Manyara, Paul Makonda ambaye ni Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo.

Wazee hao pia wamemkabidhi Mkuki na Ngao kama ishara ya kujilinda na maadui.

Aidha, wameahidi kuendelea kukiamini Chama Cha Mapinduzi pamoja na kuwa mabalozi wazuri wa kuyasemea yale yote yanayoendelea kutekelezwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2020/25.

Naye Mwenezi Makonda ametoa shukrani na kuahidi kuendelea kuwa Mwaminifu, Mtiifu na Kujituma katika kukitumikia Chama Cha Mapinduzi kwa Maslahi mapana ya Watanzania.

Leave A Reply