The House of Favourite Newspapers

Makonda Ataka Ripoti Zipatikane Ofisini Kwake Baada ya Saa 24

0

1

 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (kushoto) akizungumza na watendaji wa halmshauri za jiji la Dar es Salaam,katikati Mkuu w Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi, kulia Mkuu  Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema. 2
Mkuu wa Wilaya ya Ilala , Raymond Mushi akitoa neno la Shukrani kwa Mkuu wa Mkoa, Paul Makonda wakati wa Mkutano wa Kwanza na Mkuu wa Mkoa huyo kukutana na Watendaji, leo jijini Dar es Salaam. (Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii)

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amewagiza wakuu wa idara wa Halmashauri za Jiji la Dar es Salaam kutoa ripoti za matatizo ya wananchi na jinsi walivyojipanga ndani ya masaa 24.

Makonda ameyasema hayo wakati akizungumza na watendaji wa halmashauri hizo ikiwa ni siku ya kwanza kuingia katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa baada ya kuapishwa jana, Makonda amesema wananchi wa Dar es Salaam wanakabiliwa na changamoto za ulinzi,maji,biashara pamoja na elimu  hivyo lazima matatizo hayo yapate ufumbuzi katika kusaidia wananchi kuondokana na changamoto hizo.

Makonda amesema kuwa kwa muda alioutoa wa masaa 24 ni mkubwa hivyo lazima wafanye kazi hiyo jinsi walivyojipanga katika kutatua changamoto hizo.

Amesema wakati umefika katika kuwatumikia wananchi kuwaondolea  kero zao ambazo zinafanya kuwa na malalamiko yasioisha.

Makonda amesema amekutana na Kamanda wa Polis wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina wa Jeshi la Polisi, Simon Sirro kuzungumzanaye juu ya suala la ulinzi na usalama  kwa wananchi.

Aidha amesema kuwa kukutana huko sio mara ya kwanza ataendelea ikiwa ni lengo la kuwatumikia wananchi pamoja na kutatua kero zao.

Leave A Reply