The House of Favourite Newspapers

MAKONDA AWAAGIZA WAKUU WA WILAYA KUSIMAMIA SUALA LA LISHE

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza jambo katika mkutano huo.
Baadhi ya washiriki katika mkutano huo.
Makonda akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema (kushoto) mkataba  wa lishe. 
Makonda akiwa meza kuu.
Makonda (kulia) akimkabidhi mkuu wa Wilaya ya Temeke mkataba  wa lishe. 

 

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda amewaagiza Wakuu wa Wilaya kuweka mkazo na kusimamia ipasavyo suala la lishe katika maeneo yao na kufanya mkoa huo kuendelea kujiweka katika nafasi nzuri ya kuwa na wakazi wenye afya bora.

 

 

Makonda amesema hayo leo wakati wa kikao cha utilianaji saini wa mkataba wa lishe baina yake na wakuu wa wilaya ambapo amesema suala la lishe duni limekuwa tatizo kubwa linalopelekea matatizo ya uwezo mdogo wa kufikiri, udumavu, utapiamlo, idadi ya watoto njiti, watoto wanaozaliwa na mgongo wazi, vichwa vikubwa, uono hafifu, ukosefu wa damu, vitamin na tatizo la ukondefu.

 

 

Aidha Makonda amesema mkoa wa Dar umejidhatiti kukabiliana na tatizo la lishe kwa kutoa elimu ya lishe, kuzuia magonjwa ya upungufu wa viini lishe, kuongeza virutubisho kwenye chakula pamoja na matibabu ya utapiamlo.

 

 

Pamoja na hayo  Makonda amesema takwimu za lishe Mkoa wa Dar es Salaam mwaka 2015 zinaonyesha 14.6% sawa na watoto 91,000  kati ya watoto 624,000 wana utapiamlo (udumavu) sugu, 4.7% sawa na watoto 23,000 wana ukondefu, 59.5% sawa na watoto 371,000 wenye umri chini ya miaka 5 wana upungufu wa damu na 53.3% sawa na kinamama walio kwenye umri wa kuzaa 330,000 wana upungufu wa Damu hali inayoonyesha kuwa kuna kazi kubwa ya kufanya kukabiliana na tatizo la lishe duni.

 

 

Kwa mujibu wa wataalamu wa Afya inadaiwa athari za kudumu za ukosefu wa lishe hutokea siku 1,000 za kwanza kuanzia wakati wa ujauzito hadi pale mtoto anapotimiza umri wa miaka miwili.

Comments are closed.