The House of Favourite Newspapers

MWANAFUNZI WA SEKONDARI AGUNDUA SIMU ISIYOTUMIA VOCHA

Kijana Simon Petrus ambaye ni Mwanafunzi wa Abraham Iyambo Senior Secondary School nchini Namibia amegundua simu inayofanya mawasiliano bila ya kutumia muda wa maongezi ‘vocha’ ambapo mtumiaji wa simu hiyo, huhitaji kuwa na ‘sim card na airtime’ badala yake inatumia mawimbi ya redio.

 

Imeelezwa kwamba, Petrus ametumia miaka miwili kukamilisha ugunduzi huo alioufanya kwa kutumia mabaki ya simu na runinga zilizoharibika huku wazazi wake ambao ni maskini wakihangaika kumsaidia kijana wao katika ugunduzi wake ambao umemgharimu kiasi cha zaidi ya fedha za Kitanzania, Shilingi milioni nne.

 

Mwaka jana, nchini Namibia, kijana Gerson Mangungu aligundua mtandao wa Kijamii unaotumiwa Namhook. Miaka miwili iliyopita, Josua Nghaamwa alitengeneza mtambo wa satellite booster kwa ajili ya kurahisisha mawasiliano vijijini.

 

Katika Shule hiyo ya Iyambo, binti Adreheid Hamutumwa ametengeneza sabuni ya kuogea kwa kutumia mizizi ya miti na mafuta ya wanyama.

Comments are closed.