The House of Favourite Newspapers

Makonda: CCM Yaungana Na Watanzania Maombolezo Ya Siku 7 Za Msiba Wa Hayati Rais Mwinyi-Video

0

Katibu wa NEC itikadi na uenezi Paul Makonda amempongeza Waziri wa Ardhi Jerry Silaa kwa kazi anayoifanya ya kutatua migogoro ya ardhi hata kama utatuzi wake unamiza lakini anafanya kazi nzuri.

Makonda ameendelea kwa kusema kuwa kazi ya Waziri huyo inapaswa kuungwa mkono ili kukomesha vigogo wanaong’ang’ania ardhi za wenzao.

“Tunaungana na Watanzania wote kuendelea kutoa pole kwa misiba tuliyoipata kama Taifa kwa kipindi cha mwezi mmoja wakiwemo aliyekuwa Waziri Mkuu Mstaafu Hayati Edward Lowassa, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tabora na Mjunbe wa Halmshauri Kuu ya CCM Taifa , Pamoja na Aliyekuwa Rais wa Awamu ya Pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Al Hassan Mwinyi”

“Wana CCM wote tunaungana na Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kupindi chote cha maombolezo cha siku 7 na kuwataka kama Taifa tuendelee kushikamana ili nyakati tutakazoitwa kwa Mungu wetu tuwe hadithi njema kwa wale watakaotusimulia hapa Duniani”

Leave A Reply