The House of Favourite Newspapers

Makonda kujenga Makao Makuu ya kisasa Bakwata

0

1

Mufti Mkuu wa Tanzania, Abubakar Zuberi akizungumza jambo katika hafla hiyo.

2

Shehe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhadi Mussa Salim akimkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kwenye hafla hiyo.

3

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungunguza jambo kwenye hafla hiyo.

4

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ali Hapi (wa kwanza kushoto) akifuatilia hafla ilivyokuwa ikiendelea.

5

Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema (wa kwanza kushoto) akifuatilia hafla ilivyokuwa ikiendelea.

6

Meza kuu ilivyoonekana.

7

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akimwonesha Mufti Mkuu wa Tanzania, Abubakar Zuberi ramani ya mchoro wa jengo hilo la ghorofa tatu litakalojengwa.

8

Abubakar Zuber akikabidhiwa ramani ya mchoro wa jengo hilo la ghorofa tatu.

9

Ramani hiyo ikioneshwa mbele ya wanahabari.

10

Baadhi ya waumini wa Kiislamu waliohudhuria hafla hiyo.

11

ofia Mjema (kulia) akiagana na mmoja wa viongozi wa Kiislamu kwa upande wa akina mama.

NA DENIS MTIMA/GPL

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema kuwa anatarajia kujenga jengo jipya la ghorofa tatu kwa ajili ya Makao Makuu ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA).

Makonda amesema jingo hilo litagharimu kiasi cha zaidi ya shilingi bilioni tano za Kitanzania.

Mkaonda ameyasema hayo leo kwenye hafla iliyofanyika katika Makao Makuu ya BAKWATA, Kinondoni jijini Dar es Salaam, ambapo alienda kwa ajili ya kuzindua ujenzi wa jengo hilo jipya ambalo litajengwa maeneo hayo.

Amesema ujenzi huo unatokana na mchango mkubwa unaotolewa na BAKWATA kuhakikisha Taifa linakuwa na Amani hasa ukizingatia mkoa wake wa Dar es Salaam kuwa na idadi kubwa ya watu lakini kutokana na mchango huo wa Bakwata, kumekuwa na amani ya kutosha ndani ya jiji na hata nje.

Katika jengo hilo, kutakuwa na kumbi za kisasa ambazo zitasaidia katika shughuli zao za kupokea wageni kutoka sehemu mbalimbali na kumwezesha Mufti Mkuu wa Tanzania kufanya shughuli zake vizuri tofauti na ilivyo sasa.

Katika kuhakikisha anafanikisha ujenzi huo, Makonda amesema atafanya juhudi za ‘kujichimbia msituni’ ili kusaka fedha za kukamilisha ujenzi huo.

“Nimeona nitoe heshima kwa viongozi wangu wa dini kukabidhi ramani ya jengo hili, nitakuwa miongoni mwa watu watakaokumbukwa katika historia za kumbukumbu za vitabu vya BAKWATA katika ujenzi huo,” alisema Makonda.

Naye Mufti Mkuu wa Tanzania, Abubakari Zuber amesema anamshukuru Makonda kwa msaada wake huo, huku akiwataka watu wengine kusaidiana hata kama wana itikadi tofauti za kidini kwani kutoa msaada ni kujitolea kwa ajili ya Mungu.

Leave A Reply