Makonda Kula Sahani Moja na Wakandarasi “Janjajanja” Dar

Kufuatia kuendelea kuwepo kwa wakandarasi wanaosuasua katika ukamilishaji wa miradi ya kupunguza kero kwa Wananchi, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda ameunda timu ya wataalamu 13 kutoka Serikalini na Sekta binafsi watakaokuwa na jukumu la kupitia upya mikataba ya miradi yote ya maendeleo inayotekelezwa mkoani humo na kampuni zitakazoonekana kuenda kinyume na mikataba zitachukuliwa hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kuvunja mkataba.

 

RC Makonda amesema kumekuwa na kamchezo ka baadhi ya wakandarasi kutumia ujanjaujanja na kupenyeza rushwa ili kupata tenda huku wakidanganya kuwa wana vifaa vya kutosha lakini wanapota kazi wanashindwa kumaliza mradi ndani ya muda uliopangwa jambo linalosababisha usumbufu kwa mzigo kwa wananchi.

 

Akitolea mfano mkandarasi wa kampuni ya CHICCO Engineering iliyopewa kazi ya ujenzi wa Mto Ng’ombe, RC Makonda amesema hadi sasa kampuni hiyo imetumia muda wa 60% kazini lakini imefanya kazi ya ujenzi kwa 6% pekee licha ya kupatiwa fedha kiasi cha Shilingi Billion 4.9 huku wakazi wanaopitiwa na mto huo wakiendelea kukumbwa na mafuriko.

 

Aidha RC Makonda amesema kazi ya kuanza kupitia upya mikataba itaanza Jumanne ya March 10 na baada ya kumaliza kazi watamkabidhi ripoti maalumu pamoja na ushauri wa hatua za kuchukuwa kwa kampuni zilizoenda kinyume na mikataba ambapo tayari amegiza watendaji kuhakikisha wanamkabidhi mikataba yote.

 

Itakumbukwa mnamo mwaka jana RC Makonda aliamuru kukamatwa kwa Wakandarasi wa kampuni ya CHICCO Engineering na Nyanza kwa kushindwa kukamilisha kazi ndani ya muda uliokusudiwa lakini bado kampuni hiyo imeendelea kusuasua.ichezea.


Toa comment