The House of Favourite Newspapers

Makonda: Tuungane Na Rais Dkt. Samia Kupambana Dhulma Za Haki Kwa Wananchi

0

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Paul Makonda.

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Paul Makonda amewataka Watanzania kuungana na Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kupambana na baadhi ya Viongozi na Watumishi wa Serikali wanaodhulumu haki za Wananchi ambapo amewataka wananchi kuendelea kutoa ushirikiano wa kueleza kero, changamoto na malalamiko yao bila uwoga kwani dhamira ya Dkt. Samia ni kuwatumikia Watanzania wote pasipo kujali dini, pesa, kabila wala rangi.

“Tuungane na Mwenyekiti wa CCM na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kupambana na Viongozi na Watumishi wenye dhulma za haki za Wananchi na kuungana kwenu ni kuwa wakweli katika kusema kero na changamoto zenu ilikusudi kubaina tatizo lipo wapi na lishughulikiwe”

“Kujikosoa na kukosolewa ndio msingi na nguzo moja muhimu katika ustawi wa Chama chetu na tunabadilika na mazingira na ndio maana nikapewa mimk kuwa Mwenezi ili tuende na staili mpya na staili yenyewe sio kuhutubia bali kusikiliza kero na changamoto zenu na ndio maana tunaipeleka Serikali mhabara kujua tatizo ni nini na kutafuta dawa za kutibu”

“Tunaweza kuja hapa tukahutubia mambo mengi kumbe na nyie wananchi mna mambo yenu, tukisema tuomewe taarifa hapa utaambiwa Chama kipo imara na Serikali inafanya kazi kabisa na ndio maana wananchi wamejitokeza kwa wingi kumbe wamepakizwa magari na kuletwa hapa uwanjani, hilo hatulitaki” amesema Makonda

Leave A Reply