The House of Favourite Newspapers

MAKONDA: Yanga Njooni Mshuhudie Simba Ikichukua Kombe – VIDEO

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, amewataka mashabiki wa Simba kutokuwa na wasiwasi juu ya usalama wa kesho katika mechi ya Simba dhidi ya Kagera Sugar itakayopigwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

 

Akizungumza na Waandishi wa Habari katika Makao Makuu ya Ofisi zake zilizopo Ilala, Boma jijini Dar, Makonda ameeleza ulinzi utakuwa wa hali ya juu hivyo ni vema mashabiki wakaenda kwa wingi. Mbali na ulinzi, Makonda ameeleza kitendo cha Kombe la Bingwa wa Ligi Kuu msimu huu ambaye ni Simba kubakia Dar es Salaam ni faraja kubwa kwake akiwa kama Mkuu wa Mkoa.

 

Vilevile Makonda amesema uwepo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli atakayewakabidhi Simba kombe ni jambo kubwa kwakuwa hajawahi kuhudhuria mechi yoyote ile ya ligi. Mkuu huyo wa mkoa hajawasahau watani zake wa jadi Yanga kwa kuwakaribisha katika mechi hiyo itakayoanza majira ya saa 8 na robo mchana kesho Jumamosi.

Comments are closed.