The House of Favourite Newspapers

Makundi Ya Hip Hop Bongo Yamepoteza Msisimko

0

KIBONGOBONGO wasanii wengi wa Muziki wa Hip Hop wamekuwa wakifanya muziki huo bila kuelewa chimbuko hasa ulipotoka.

Iko hivi, harakati za Muziki wa Hip Hop zilianza kuchomoza miaka ya 1970 mitaa ya South Bronx katika Jiji la New York, Marekani na miongoni mwa waasisi wake wakiwa ni DJ Kool Herc, Grandmaster Flash na Afrika Bambaataa mwenye asili ya Jamaika.

Eneo la New York lilikuwa maarufu sana miaka ya 1980 katika nyanja ya Muziki wa Hip Hop huku mastaa kadhaa kama Run-DMC, LL Cool J, KRS- One, Doug E Fresh, Rakim, Big Daddy Kane na wengine wengi wakiufanya mji huo uliopo East Side uwe juu kwenye miondoko ya Hip Hop.

Baada ya New York kutambulisha wasanii wake kwenye ramani ya Hip Hop, mwaka 1986, Ice-T kutoka Mtaa wa Crenshaw uliopo Los Angeles, Marekani ambapo ni West Side akaachia ngoma yake ya kwanza ya 6 In The Morning na hivyo ikaanza kukosolewa vikali na upande wa pili (East Side). Baada ya kuachia ngoma yake hiyo, Ice-T akiwa na rafiki zake Jerry Heller na Eazy-E wakaunda ‘record label’ iliyojulikana kwa jina la Ruthless Record.

 

Baadaye kidogo wakatoa Albamu ya Panic Zone ambapo kundi lao walilipa jina la N.W.A (Niggaz With Attitude) humo ndani alikuwepo Arabian Prince, Eazy – E na mkali Ice Cube. Hata hivyo kutokana na masuala ya kifedha kundi hilo lilikuja kuvunjika baadaye na Eazy- E akabaki kuwa meneja wa record label ya Ruthless Record.

 

Baada ya muda record label sasa zikaanza kuenea maeneo ya West Side ambapo Dr Dre naye akaanzisha record label yake ya Death Row akiwa na Suge Knight na kuachia Albamu ya The Chronic iliyoweka heshima katika muziki huo na kusababisha wakali wengi kusainiwa katika lebo yake hiyo wakiwemo Snoop Doggy Dogg, Tupac Shakur, Warren G, The lady of Rage, Nate Dogg, Daz Dillinger na Kurupt.

Tukiachana na historia hiyo, Kibongobongo kulikuwa na makundi mengi yaliyoteka muziki huo na kuleta msisimko kama vile Kwanza Unit (KU) ya kina Chief Rhymson, Kibacha ‘KBC’, Bugzy Malone, Zomba, D-Rob na Eazy B kuna X Plastaz lililokuwa likiundwa na Zigilah, Father Nelly na wenzake.

 

Mengine ni Hardcore Unity lililoundwa na JCB, Lord Eyez, Spack Dogy na Chief Mastiff, Nako 2 Nako lililokuwa na Lord Eyez, Bou Nako, G Nako na Ibra Da Hustler kuna East wabunifu katika kazi zao kama ilivyokuwa zamani, ukisikiliza Chemsha Bongo kutoka Albamu ya Funga Kazi ya HBC kisha Ngangari na Asali wa Moyo za Gangwe Mobb utagundua ninachomaanisha.

 

Pia ukijaribu kuangalia Hip Hop Bongo ya miaka ya 90 na mwanzoni mwa miaka ya 2000 kisha ukafananisha na ya sasa, utagundua ladha ya muziki huo imeanza kushuka taratibu. Msisimko ule wa mwanzo hakuna tena yaani unapungua siku hadi siku, ushindani na mlipuko wa makundi umekuwa si kama wa zamani.

 

Wengi wamekuwa wakifanya muziki huo kikawaida na hata makundi yaliobaki yanashindwa kuleta ushindani wao kwa wao. Kundi la Weusi linaloundwa na (Joh Makini, Nikki wa Pili, G Nako na Bonta) kidogo lilianza kuonesha kuleta msisimko lakini kwa sasa limepunguza kasi.

Ukisema utaje makundi ya Hip Hop kwa sasa yaliobaki utazungumzia Weusi, muunganiko wa Roma na Stamina (Rostam), Navy Kenzo (Aika na Nahreel), OMG (Young Lunya, Quick Racka, Salmin Swagg na Con Boi), Central Zone (Moni, Slim Sal), Pah One (Igwe, Ola)… Mwandishi wa Makundi ya Coast Team ya King Crazy GK, AY, Mwana Fa, O Ten, Wateule la Mchizi Mox, Jay Moe, Solo Thang, Hard Blasters Crew (HBC) lililokuwa na Terry (Fanani), Nigga J (Prof. Jay) na Big Willy (Crazy One), Chamber Squad la Ngwea, Dark Master, Noorah na Mez B. Mengine ni Gangwe Mobb, GWM, TMK Wanaume Family, Wagosi wa Kaya, Mabaga Fresh, The Diplomatz, Manduli Mobb, University Corner na Manzese Crew.

Katika makundi hayo ya Kibongo, mengi yamekufa na yaliobaki kwa sasa ni machache sana ambayo ni Wagosi wa Kaya, TMK Wanaume Halisi, Mabaga Fresh na wengine wamekuwa wakifanya muziki huo peke yao (solo). Wengi wao wamekuwa..Kaisome zaidi kwenye Gazeti la Ijumaa leo.

MAKALA NA ANDREW CALOS

Leave A Reply