The House of Favourite Newspapers

Makusu Afungukia Dili Lake Yanga

0

MSHAMBULIAJI wa zamani wa Orlando Pirates na AS Vita, Jen Marc Makusu Mundele, ameweka wazi kuwa kwenye mazungumzo na uongozi wa Yanga huku mwenyewe akisema kuwa yupo ayari kujiunga na timu hiyo kama
mazungumzo yatakwenda sawa.

 

Makusu Mundele ambaye anamudukucheza nafasi zote za mbele, anakumbukwa kwa ubora mkubwa ambao
amewahi kuuonyesha akiwa na AS Vita ya nchini DR Congo ambapo alifanikiwa kuwa mfungaji bora wa timu hiyo katika msimu wa mwaka 2018/19 ambapo alifunga mabao 20.

 

Kuelekea katika dirisha dogo la usajili ambalo limefunguliwa rasmi leo Desemba 15, Yanga inaruhusiwa kufanya usajili wa wachezaji wengine wawili kutokana na kuwa na wachezaji 10 pekee wa kigeni huku wakiruhusiwa kuwa na idadi ya wachezaji 12 wa kigeni kwa mujibu wa bodi ya ligi kuu.

 

Akizungumza na Championi Jumatano, Makusu alisema kuwa, tayari amefanya mazungumzo na uongozi wa Yanga na anachosubiri kwa sasa ni kuona dili hilo linakamilika kwa upande wa viongozi wa timu, wakimalizana yeye hana tabu na yupo tayari kujiunga na Yanga.

 

“Yanga tayari mazungumzo yamekwishafanyika, tayari tumewasiliana na kuna mambo ambayo lazima wamalizane na uongozi wangu na uongozi wa timu hivyo nasubiri kuona kama watakamilisha basi mimi sitakuwa na tatizo kujiunga na Yanga.

 

“Yanga ni timu nzuri na kuna marafiki zangu wengi pale ambao nimekuwa nikiwasiliana nao mara
kwa mara, Djuma Shabani na Yanick
Bangala tumekuwa tukiwasiliana kwa muda mrefu na wao wanatamani
mimi kuwa mmoja wa wanafamilia
wao,” alisema mshambuliaji huyo.

Stori na Marco Mzumbe, Championi Jumatano

🔴#LIVE: MASHINE MBILI ZA SAINI SIMBA, CHAMA AKIWEPO, NABI AANZA KUPEWA VITISHO | KROSI DONGO

Leave A Reply