The House of Favourite Newspapers

Malaika Amfungukia Pam D

0

 

MKALI wa ngoma za Saresare pamoja na Zogo, Diana Exavery ‘Malaika’ amefunguka kuwa  mashabiki wa muziki wamekuwa wakimfananisha staili yake ya uimbaji na mwanamuziki mwenzake Pamela Daffa ‘Pam D’ kutokana na wote kufanya kazi katika studio moja tena zinazofanywa na prodyuza yuleyule.

Akipiga stori na Showbiz, Malaika alisema yeye na Pam D hawafanani kabisa sauti lakini staili yao ya uimbaji inaonekana kuwa sawa kwa mashabiki wao kwa sababu ya ngoma zao kutengenezwa na Prodyuza Mensen Selekta ambaye tayari amejitengenezea ‘identity’ yake katika utengeneza wa nyimbo.

“Mimi na Pam wote tunafanya kazi kwa Mensen na utengenezaji wake wa nyimbo unajulikana. Ukizisikiliza biti za Mensen unaweza kuona kama zinaendana hivi lakini kiukweli kwa wanaonifananisha na Pam naomba niwaambie watusikilize vizuri na wataweza kugundua kuwa tunatofauti kubwa,” alimaliza Pam D.

Stori: Ally Katalambula | UWAZI | SHOW BIZ

LIVE: Mapokezi ya Muigizaji ‘Cloud’ 112, Dar Akitokea Sweden Yavunja Rekodi

Leave A Reply