The House of Favourite Newspapers

Malaika Napenda Muziki Kuliko Filamu

0

Ukiambiwa utaje listi ya mastaa wa kike ambao wanafanya vizuri kwenye gemu ya muziki wa Bongo Fleva, basi naamini kabisa kuwa huwezi kuacha kutaja jina la mwanadada Diana Exavery ‘Malaika’ ambaye amewahi kutamba na ngoma zake kama Rarua, Zogo na nyingine kibao.

 

Amani limemtafuta na kupiga naye stori nyingi ambapo amefunguka mambo mengi kuhusu maisha yake ya uhusiano na sababu za ukimya wake kwenye gemu ya muziki, ungana nami hapa chini kwa mahojiano kamili.

 

Amani: Umekuwa kimya kwa kipindi kirefu, sababu kubwa ni nini?

 

Malaika: Ni kweli tangu niachie ngoma yangu mpya ya Baila ni zaidi ya miezi saba sasa, lakini hii haimaanishi kwamba nimeacha kuimba hapana, kuna muda msanii unatakiwa utulie kwa kupindi fl’ani, ili hata utakaporudi uwe na kitu kipya ambacho mashabiki watakipenda zaidi, kwa hiyo naomba tu mashabiki zangu waendelee kuwa wavumilivu kwa sababu kuna vitu vingi vizuri nimewaandalia.

 

Amani: Watu wengi wanafahamu kuwa ngoma ya Uswazi ndiyo iliyokutambulisha zaidi kwenye jamii, je, baada ya hapo ilikupa mianya gani kwenye muziki?

Malaika: Uswazi ilinifungulia njia kwa sababu nilifanya na msanii mkubwa tayari ambaye ni Chege mwenyewe, hivyo nikaanza kujulikana zaidi na kufungua njia ya kazi zangu mwenyewe.

 

Amani: Unamzungumziaje Chege kama mtu aliyekutambulisha kwenye gemu?

 

Malaika: Chege ni kama kaka yangu na ninaweza kumuita baba yangu kwenye muziki, chochote ninachokifanya kuhusiana na muziki huwa namshirikisha na ananisapoti sana hata kipindi nipo kimya, alikuwa akiniuliza kama kuna shida.

 

Amani: Umetambulika na ngoma ya Uswazi Take Away na mpaka sasa bado unaendelea kuachia kazi zako ukiwa mwenyewe, vipi unayaonaje mapokezi ya mashabiki zako?

 

Malaika: Kiukweli nisiwe mnafki tangu nimeanza kuachia ngoma zangu mwenyewe na hata zile ambazo nimeshirikiana na wasanii wengione naona mashabiki zangu wanaendelea kunipokea vizuri.

Amani: Je kwa mtu anayefuatilia kazi zako anazipata vipi kwenye platforms?

Malaika: Mwanzo kipindi naanza sikuwa na YouTube chanel, ila nilipotoa kazi zangu mbalimbali ikiwemo na ngoma ya Baila ilipata karibu wafusi laki mbili (27k) sio kitu cha kawaida kwa mtu ambaye anaanza kumiliki chaneli.Amani: Umekuwa taratibu sana katika kuachia ngoma vipi hiyo ndio staili yako uliyoichagua?

 

Malaika: Ni changamoto za wasanii wa kike katika kuhakikisha anafikisha kazi nzuri na kupanda kila siku huwa nathamini sana kutoa kazi nzuri kwa mashabiki zangu.

 

Amani: Unaionaje tasnia ya muziki wa Bongo Fleva kwa sasa?

 

Malaika: Gemu limebadilika maana niliwahi kukaa miaka minne kimya lakini tangu niliporudi naona mabadiliko makubwa, hata wasanii wa kike nao wameongezeka kwa wingi tena wanafanya vizuri sana soko

 

Amani: Ulikuwa nje ya gemu kwa muda mrefu, vipi bado unaoana status yako ipo palepale?

Malaika: Bado nipo kwenye status yangu hata nilipokuwa kimya mashabiki walikuwa wakiuliza niko wapi nirudi.

 

Amani: Mipango yako iko vipi maana kila kukicha zinaibuka kazi mpya za wasanii wengine nawe uko slow(taratibu)

 

Malaika: Mipango na mikakati ni kufanya kazi nyingi ambazo zitawafikia mashabiki na kama nilivyosema hapo mwanzo kuwa kuna vitu vingi bado vipo jikoni hivyo mashabiki zangu waendelee kukaa mkao wa kula.

Amani: Hujaonekana kufanya kazi na wasanii wa kike, je shida nini?

 

Malaika: Kama timu yangu tuna imani ya kufanya kazi nyingi tu na wasanii wa kike.

Amani: Uliwahi kuonekana kwenye filamu pia lakini baadaye ukapotea, kitu gani kilitokea?

 

Malaika: Siendelei na kucheza filamu maana niliitwa ni kwa heshima ya Mzee Kambi, alikuja kuniomba kutokana na uhusika tu, Ndoto yangu kubwa ni kwenye muziki na si filamu na ndiyo maana bado naendelea kuachia ngoma tu.

 

Amani: Tukirudi kwenye maisha yako binafsi, umekuwa ni msanii ambaye hupendi kuweka mambo ya mahusino yako hadharani kwanini?

 

Malaika: Unajua nipo kwa ajili ya kuwapa mashabiki muziki mzuri na si mambo yangu binafsi, hivyo ndio maana mara nyingi sipendi watu wamjue mtu ninayetoka naye kimapenzi hii inasaidia hata kuwafanya watu wasikuongelee zaidi.

 

Amani: Unaweza vipi kuepukana na usumbufu wa wanaume wa kware ukizingatia wewe ni msichana mrembo?Malaika: Usumbufu upo kwa mwanamke yeyote, muhimu ni kujitambua tu na mimi niko kwenye uhusiano hivyo namheshimu niliyenaye.

 

Amani: Mipango ya ndoa imekaa vipi kwa upande wako?Malaika: Ndoa ni kitu cha heri na huwa kinatokea kwa mtu yeyote.

 

Amani: Umerudi na utofauti hasa kwenye urembo wako, Nini kilikusukuma kufanya teeth braces(urembo wa meno)?

Malaika: Hii ilikuwa ni kiu yangu kutengeneza urembo wa meno ili kupata tabasamu zuri na mpangilio mzuri wa meno yangu.Amani: Je haupitii changamoto yoyote?

 

Malaika: Changamoto kubwa ni watu wanakuwa wananishangaa ila mimi naona kama ni kitu cha kawaida.Amani: Marekebisho hayo yamekugharimu kiasi gani cha pesa?

 

Malaika: Imenigharimu kiasi cha milioni nne za kitanzania na hii ni bei ndogo tu kwa hapa kwetu ila nchi za wenzetu wanazingatia sana.Amani: Mafanikio gani ambayo unaweza kujivunia kupitia kazi yako ya muziki?

 

Malaika: Mara nyingi sipendi kutaja mafanikio japo yako mengi maana sitaki kuwaharakisha vijana hasa wa mashuleni.

Leave A Reply