The House of Favourite Newspapers

Malawi Yamuomba Tyson Kuwa Balozi Wake wa Bangi

0

WIZARA ya Kilimo ya Malawi imemwandikia barua bingwa wa zamani wa ndondi duniani, Mike Tyson ikimuomba kuwa balozi wa bangi nchini humo kwa ajili ya matumizi ya tiba na biashara.

 

Katika barua yake, Waziri Lobin Lowe amesema kuhalalishwa kwa bangi mnamo 2020 kumeunda fursa kimataifa na kwamba kwa kushirikiana na Jumuiya ya Bangi ya Marekani lengo lao ni kuwezesha mpango huo na Tyson unafanikiwa.

 

“Malawi inaweza isijiendeshe peke yake kwani tasnia hii ni ngumu inayohitaji ushirikiano. Kwa hivyo ningependa kukuteua, Mike Tyson, kuwa Balozi wa Tawi la Bangi la Malawi,” Lowe aliandika.

 

Ikumbukwe kuwa, Tyson pia ni mjasiriamali na amewekeza katika kilimo cha bangi. Vyombo vya habari nchini humo viliripoti kwamba Tyson alitarajiwa nchini Malawi wiki iliyopita lakini ziara yake iliahirishwa.

Leave A Reply