The House of Favourite Newspapers

Malkia Karen Amwaga Machozi Kanisani Ibada Ya Kusalia Mwili Wa Baba’ke KKKT Usharika wa Mbezi – Video

0


WANANCHI wamejitokeza katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Mbezi Beach Jumanne Aprili 22, 2024 kwenye ibada ya kuuombea mwili wa Gardner Habash aliyekuwa mtangazaji wa Clouds Media kipindi cha Jahazi.

Gardner amefariki dunia Aprili 20, 2024 katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Dar es Salaam alipokuwa anapatiwa matibabu.

Baada ya ibada hiyo mwili utapelekwa viwanja vya Leaders Club kwa ajili ya kuagwa na kupelekwa uwanja wa ndege kwa safari ya kuelekea kijijini kwao Wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya mazishi yatakayofanyika kesho Jumanne Aprili 23, 2024.

Baada ya ibada ya kuuombea mwili wa Gardner Habash aliyekuwa mtangazaji wa Clouds Media kumalizika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Mbezi Beach, safari imeanza kuelekea viwanja vya Leaders Club kwa ajili ya kuagwa.

Baada ya hapo mwili unatarajiwa kupelekwa uwanja wa ndege kwa safari ya kuelekea kijijini kwao wilayani Rombo Mkoa wa Kilimanjaro kwa ajili ya mazishi yatakayofanyika kesho Aprili 23, 2024.

Leave A Reply