The House of Favourite Newspapers

Malkia Karen: Baba wa Mtoto Mnampa Ninyi?

0

MSANII wa kike wa Bongo Fleva, Careen Gardner almaarufu Malkia Karen anasema kuwa, anawashangaa mno watu wanaompangia mtoto wake baba, jambo ambalo linamuumiza kwani kama ni mtoto amezaa yeye mwenyewe.


Akizungumza na
Gazeti la Ijumaa juu ya ishu hiyo, Malkia Karen ambaye ni mtoto wa mtangazaji maarufu wa Clouds FM, Gardner G Habbash anasema kuwa, anaumia mno kila kukicha kutokana na mtoto wake aliyejifungua hivi karibuni kupewa baba wakati ukweli anaujua yeye mwenyewe.


“Jamani tangu
nikiwa mjamzito baba wa mtoto mnanipa ninyi? Mtu anakupangia mtoto, kweli ni sahihi hiyo?
Mimi ni mama na
mimi najua wazi baba wa mtoto ni nani hivyo wasinipangie kabisa, wanakosea sana.


“Mtoto wangu ipo
siku atakuwa na kuona hayo, sidhani kama atapenda kwa kweli,” anasema Malkia Karen ambaye
baba wa mtoto wake
amekuwa akihusishwa na mastaa kama Diamond Platnumz na Rayvanny.


Lakini Gazeti la
IJUMAA linafahamu kwamba mtoto huyo siyo wa mastaa wanaotajwa bali ni wa jamaa ambaye siyo
staa na ni mfanyakazi
wa serikalini asiyependa mambo ya mitandaoni kutokana na aina ya kazi yake.

STORI; IMELDA MTEMA, DAR

#LIVE: RAIS SAMIA ALIVYOAGWA MISRI BAADA YA KUMALIZA ZIARA YAKE, APANDA NDEGE KURUDI NCHINI..

Leave A Reply