The House of Favourite Newspapers

MALKIA KAREN; ‘Mgonjwa’ wa Juisi ya Miwa!

0
Bongo Fleva, Karen G Habash ‘Malkia Karen’.

MAMBO vipi msomaji wa safu hii ya My Style, kama ilivyo kawaida huwa tunakutana na mastaa mbalimbali nchini ili kuzungumzia maisha yao binafsi mbali na sanaa, mahusiano na vitu vingine vingi.

 

Leo tupo na msanii chipukizi na anayefanya poa kunako gemu la Bongo Fleva, Karen G Habash ‘Malkia Karen’ ambaye kwa sasa anatamba na wimbo wake wa Tabu ambapo katika mahojiano haya amefunguka mambo mengi usiyoyajua:

 

My Style: Ukiamka jambo gani huwa ni la kwanza kulifanya? Karen: Jambo la kwanza pindi ninapoamka kitandani ni kwenda kuoga, kisha baada ya hapo nafanya usafi chumbani kwangu nikimaliza ndio ratiba zingine zinafuata, ila sio mpenzi sana wa kunywa chai.

My Style: Kwa nini hupendi kunywa chai?

Karen: Sio mpenzi wa kunywa chai kwa sababu mara nyingi asubuhi huwa nakuaga na vitu vingi vya kufanya, hivyo unakuta nipo bize nahangaikia hiyo ishu na kujikuta muda umeenda. Mara nyingi huwa nakunywa chai siku
za Jumapili nikiwa nimetulia tu nyumbani.

My Style: Asilimia kubwa ya watu huwa wanadhani kwamba mtu asiyependa kunywa chai asubuhi basi anatumia kilevi, hii kwako imekaaje?

Karen: Hapana, inategemea. Mfano kama mimi mara nyingi nyumbani huwa nakua peke yangu watoto wanaenda shule, wazazi kazini hivyo nakuwa naona uvivu wa kuanza kutengeneza chai ndio maana huwa sinywi. My Style: Starehe yako kubwa ni nini?

Karen: Starehe yangu kubwa ni kusikiliza muziki.

My Style: Ukiwa na msongo wa mawazo huwa unapenda kufanya nini?

Karen: Kwanza sipendi kabisa kukaa mwenyewe hata sehemu iwe nzuri kiasi gani, mara nyingi nikiwa na msongo
wa mawazo huwa napenda kukaa na rafiki zangu ili kujaribu kuiondoa ile hali.

 

Tunakuwa tunashea mambo mengi ambapo mwisho wa siku tutatoka kwenda sehemu fl’ani na kujikuta nasahau mawazo yote.

My Style: Viwanja vyako vikubwa vya starehe kwa hapa Bongo ni vipi?

Karen: Mimi sio mtu wa kutoka sana, hivyo mara nyingi nakuwa nipo nyumbani na nisipokuwa nyumbani basi nitakuwa studio au kwenye biashara zangu.

My Style: Aina gani ya nguo ukivaa unahisi ndio unatokelezea zaidi? Karen: Napenda sana kuvaa suruali ya jinzi na shati ndio nakuwa comfortable zaidi kuliko nikivaa nguo zingine.

 

My Style: Msanii gani hapa Bongo ambaye huwa unamuangalia kama mfano wa kuigwa na jamii?

Karen: Lady Jaydee, kwa sababu ni msanii ambaye anaangaliwa na vijana wengi wa kike kwa kiume. Ni msanii ambaye jina lake na heshima yake bado vipo, pia hata life style yake ya muziki inamvutia kila mtu.

My Style: Vipi kwenye mavazi? Msanii gani mapigo yake yanakuvutia zaidi? Karen: Kwenye mavazi ni Vanessa Mdee, yupo unique halafu anapendeza sana.

My Style: Unapendelea chakula na kinywaji cha aina gani?

Karen: Napenda ugali, dagaa, matembele na kachumbari sana, pia katika vinywaji napenda sana kunywa juisi ya miwa yaani haiwezi kupita siku sijanywa.

My Style: Unapenda rangi gani ya nguo? Karen: Awali nilikuwa napenda sana kuvaa crazy colours (mchanganyiko wa rangi nyingi) lakini siku hizi naona napendeza sana nikivaa nguo nyeusi.

My Style: Unaweza kutoka ukiwa hujapaka make up?

Karen: Ndio naweza ila inategemea na sehemu yenyewe kwa sababu kuna sehemu zingine inakubidi upake make up ili uendane na tukio.

My Style: Unapokuwa nyumbani mara nyingi huwa unapenda kufanya nini?

 

Karen: Mara nyingi huwa napenda kufua nguo zangu na kupika chakula.

My Style: Unapenda kuwa na mwanaume wa aina gani? Karen: Napenda mwanaume ambaye ataweza kunisapoti kwenye kazi zangu, awe na hofu ya Mungu, lakini pia aipende familia yangu.

My Style: Ukiwa unatoka na mpenzi wako unapenda awe katika muonekano upi wa mavazi?

Karen: Napenda awe smart yaani avae nguo yoyote ambayo itaendana na sehemu tunayoenda.

My Style: Unatembelea gari ya aina gani na ipi ni gari ya ndoto yako?

Karen: Kwa sasa sina gari, ila gari ya ndoto yangu ni BMW.

My Style: Unatumia perfume gani? Karen: Natumia splash za Victoria Secret.

My Style: Una mpango wa kuolewa lini na kama ukibahatika ndoto yako ni kuja kuwa na watoto wangapi? Karen: Napenda kuwa na watoto watatu na kuhusu ndoa siku yoyote Mungu akipenda.

Leave A Reply