The House of Favourite Newspapers

Shamsa Ateswa na Dola 100 za Chid Mapenzi

0

MUIGIZAJI Shamsa Ford amesema japo muda mrefu kidogo umepita tangu aachane na mumewe, Rashid Said ‘Chid Mapenzi’, lakini bado anakumbuka alivyomdai Dola 100 alizompa kwa ajili ya kuongeza ada ya mtoto wake.

 

Akizungumza kwa uchungu, Shamsa amesema kilichomfanya afikie hatua ya kuachana kabisa na mumewe huyo ni kitendo cha kuonesha kutomjali mwanaye ambaye alizaa na mwanaume mwingine, Dickson Matoke.

 

“Siku hiyo Chid alinipa Dola 100 kuniongezea ada ya mtoto sasa kuna siku tuligombana akanidai tangu siku hiyo nilimtoa moyoni na mpaka sasa nikimkumbuka naumia sana,” alisema Shamsa.

 

Shamsa na Chid walifunga ndoa huku kila mmoja akionesha kumpenda mwenzake vilivyo, lakini baada ya mwaka mmoja walitengana na sasa kila mtu ana maisha yake.

STORI NA IMELDA MTEMA | GPL

Leave A Reply