The House of Favourite Newspapers

Mama Adaiwa Kumzika Mtoto Wake Akiwa Hai

Polisi katika Wilaya ya Apac nchini Uganda wameanza uchunguzi dhidi ya mwanamama anayedaiwa kumzika akiwa hai mwanaye wa kiume mwenye umri wa miezi miwili.

 

Imeelezwa kuwa Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 19 mkazi wa kijiji cha Awiri katika Parishi ya Kidilani katika mji wa Chegere alichimba kaburi na kumzika mwanaye siku ya jana (Jumatatu).

 

Imesemekana kuwa mwanamke huyo alifikia hatua hiyo baada ya wazazi wake kumnyima chakula wakidai kuwa amezaa mtoto haramu.

 

Mmoja wa wakazi wa eneo hilo ameeleza kuwa mtuhumiwa huyo alitoweka na mtoto wake nyumbani kwao kwa muda wa siku tatu na aliporudi siku ya Jumatatu hakuwa amerudi naye. Vyombo vya usalama wilayani humo vimethibitisha kujiri kwa tukio hilo na kusema kuwa vinaendelea na uchunguzi.

 

Imearifiwa kuwa baada ya kuulizwa kueleza alipo mtoto wake, mwanamke huyo alikiri kuwa amemzika akiwa hai, na kudai kuwa ni baada ya yeye na mwanaye kutengwa na familia yake. Mtuhumiwa huyo anashikiliwa katika Kituo cha Polisi Apac

Chanzo: Jamiiforums

Comments are closed.