The House of Favourite Newspapers

Wasanii Wamualika Mama Maria Tamasha la Mwalimu

Mtoto wa Mwalimu Nyerere, Makongoro Nyerere akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani)

Wasanii wa tasnia mbalimbali nchini, wamtembelea Mama Maria Nyerere nyumbani kwake, Msasani jijini Dar kumsalimia na kumualika kwenye Tamasha la Kumbukumbu ya Miaka 20 ya Mwalimu Nyerere.

Akizungumza na waandishi wa habari leo nyumbani hapo, Simon Mwakifamba ambaye ni Rais wa Shirikisho la Filamu alisema mbali na kumjulia hali pia wanatumia fursa hiyo kumualika kwenye tamasha hilo.

“Tamasha litafanyika kwenye Ukumbi wa Mwalimu Nyerere na baadaye mkesha utafanyika kwenye Ukumbi wa Mwalimu Nyerere siku ya Ijumaa ambapo mgeni rasmi atakuwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Pombe Magufuli na viongozi wengine.

“Tamasha hili limeandaliwa na wasanii na litakuwa na burudani kutoka kwa wasanii wa  Bongo Fleva, Sengeli, Maonesho, Gospo na Mashairi,” alisema Mwakifwamba Kwa upande wake, mtoto wa Mwalimu Nyerere, Makongoro Nyerere alisema wapo tayari kushiriki tamasha hilo.

Na Neema Adrian

Comments are closed.