The House of Favourite Newspapers

Mama alivyoua wanaye kwa sumu

0

ELIZA BUGUSI STEVEN]ALIYEWAUA WATOTO WAKE KWA SUMU-001 Eliza Bugusi Steve, enzi za uhai wake.

Stori: Gregory Nyankaira, UWAZI

MARA: Mwanamke mmoja Eliza Bugusi Steven (28), mkazi wa Kijiji cha Kamugegi, Kata ya Kamugegi, Wilaya ya Butiama mkoani Mara, ameelezewa jinsi alivyowaua kwa kuwanywesha sumu watoto wake wawili wa kuwazaa.

MAREHEMU NICHLOUS STEVEN[4] ALIYEUAWA-001Nicholaus Steven (miaka 4)

Mashuhuda wa tukio hilo wameeleza kuwa Eliza alifanya tukio hilo Januari 7, mwaka huu, saa nne usiku akiwa nyumbani kwao, kwa kile kilichodaiwa kunyanyapaliwa na ndugu zake baada ya mwanamke huyo kurejea kuishi kijijini akitokea jijini Mwanza alikokuwa akiishi na mumewe.

MTOTO FRANCIS STEVEN]2] ALIYEUAWA KWA SUMU NA MAMA YAKE-001Francis Steven (miaka 2)

Marehemu hao, Nicholaus Steven (4) na Francis Steven (2) walinyweshwa sumu hiyo iliyokuwa kwenye kikombe na baada ya kuhakikisha wamepoteza uhai, mwanamke huyo naye alikunywa iliyobaki, lakini akaokolewa muda mfupi baadaye baada ya kupiga mayowe ya kuomba msaada.

waombolezaji-001Waombolezaji siku ya msiba

Inadaiwa kuwa, Eliza ambaye mumewe alifariki dunia mwaka jana, tangu alipofika kijijini hapo amekuwa akinyanyapaliwa na mama yake mzazi pamoja na mdogo wake, ambao wamekuwa wakimtuhumu kuugua ugonjwa unaotokana na ngono.

Diwani wa Kata ya Kamugegi, Ikungura Charles, amesema: “Mdogo wa Eliza ambaye aligombana naye muda mfupi kabla ya tukio hilo, ametoweka nyumbani hapo.”

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mara, Philipo Kalangi amethibitisha kuwepo kwa tukio hilo.

“Mtuhumiwa atafikishwa  mahakamani kwa kosa la mauaji na jaribio la kujiua baada ya hali yake kutengemaa,” alisema kamanda huyo.

Leave A Reply