The House of Favourite Newspapers

Mama Awapa Sumu Wanaye Watano, Wawili Wafariki Dunia

0

Jeshi la Polisi mkoani Geita, linamshikilia mwanamke mmoja, Veronica Gabriel (30), mkulima wa Kijiji cha Mwabagaru, Kata ya Buseresere mkoani Geita kwa tuhuma za kuwawanywesha sumu watoto wake watano na kusababisha wawili kati yao kufariki dunia.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Henry Mwaibambe, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa mwanamke huyo aliwanyweshwa wanaye hao sumu ya kuua wadudu kwenye zao la nyanya kisha na yeye kunywa kwa kile alichodai kuwa ni kuchoshwa na ugumu wa maisha.

Kamanda Mwaibambe amesema kitendo hicho kilisababisha wawili kati yao wapoteze maisha huku wengine watatu pamoja na mama yao wakiendelea na matibabu katika Kituo cha Afya Bwanga, hali zao zikiwa ni mbaya.

Ameongeza kuwa mtuhumiwa huyo yupo chini ya ulinzi wa Jeshi la Polisi na uchunguzi zaidi kuhusu tukio hilo unaendelea.

Leave A Reply