The House of Favourite Newspapers

Mama Kanumba Afanya Yake Stendi ya Mabasi

MAMA wa aliyekuwa mwigizaji kinara wa Bongo Movies, marehemu Steven Kanumba, Flora Mtegoa, kama kawaida yake ameangua kilio cha nguvu kwenye Stendi ya Mabasi ya Segerea jijini Dar, baada ya kuona bango kubwa la mwanaye huyo kwenye duka moja eneo hilo.

 

Akizungumza na Gazeti la Ijumaa Wikienda kwa uchungu, mama huyo alisema kuwa, siku hiyo alikuwa anakwenda kurekodi filamu maeneo ya Segerea na alipofika kituoni hapo, alishuka kwenye basi ndipo ndipo akakutana uso kwa uso na picha kubwa ya mwanaye huyo.

 

“Kila mara naziona picha za Kanumba kwenye mabango, lakini sijui ni kwa nini hii nilipoiona, imenifanya niishiwe nguvu,” alisema mama huyo.

Na Imelda Mtema | Ijumaa Wikienda

Usiku wa Vikings Waibua Mazito Wema, Aunt, Wolper!

Comments are closed.