The House of Favourite Newspapers

Mama Kija ya Tunda Man nyuma ya pazia

0

TUNDA copyAndrew Carlos

KILA staa wa Bongo Fleva hivi sasa ameelekezea kutoka kimataifa ili kujitambulisha na kuitambulisha nchi na pia wapo mastaa wengine wa Bongo Fleva ambao wanaamini kutengeneza video nzuri na mazingira mazuri ni nje ya nchi hasa kwa nchi za Nigeria na Afrika Kusini.

Zipo baadhi ya video ambazo zimetengenezwa nje ya nchi kama vile Ningefanyaje ya Ben Pol, Don’t Bother ya Joh Makini, Nana ya Diamond, No Stress ya Linah na nyingine nyingi.

Katika hali hiyo imekuwa tofauti kwa staa wa Bongo Fleva, Khalid Ramadhan ‘Tunda Man ambaye anaamini bado video na mazingira mazuri yanapatikana Bongo.

Staa huyo aliyewahi kubamba na ngoma kadhaa kama vile Achana na Mimi, Neila, Msambinungwa na nyingine nyingi mwezi uliopita aliachia video ya ngoma yake mpya inayo-tambulika kama Mama Kija akimuelezea mwanamke mwenye ujauzito ambaye analazimisha kupata kila anachokitaka kiasi cha kumsumbua mumewe.

Mtandao hmefanikiwa kunasa picha za video hiyo ambazo ni nyuma ya pazia.

Leave A Reply