The House of Favourite Newspapers

Mama Lishe Wachuana Kupika Chapati, Utashangaa!

0
Wakikoleza moto.

AKINAMAMA Lishe wa Soko la Ilala jijini Dar es Salaam, leo Ijumaa, Aprili 3, 2020, wametoana jasho katika Shindano la Kupika Chapati lililoendeshwa na Makampuni ya Azania Group kwa kushirikiana na Makampuni ya Global Group.

 

Wakikanda unga.

 

Katika shindano, akinamama hao walitumia unga bora wa ngano wa Azania pamoja na mafuta ya kupikia ya Azania Fresh ambayo ndiyo habari ya mjini kwa sasa kutokana na ubora wake hasa kwenye mapishi ya vyakula kama chapati, maandazi, keki, bagia, sambusa, na vyakula vinavyofanana na hivyo.

 

Mapishi yameanza.

 

Mama Lishe hao kila mmoja alionyesha umahiri wake na kutoa kitu bora ambapo baada ya kukamilika kwa zoezi la upikaji, chapati hizo ziligawiwa kwa mashuhuda waliojitokeza kujionea mpambano huo wa kihistoria.

 

Mama Lishe akionyesha umahiri wake.

 

Baada ya kuzionja chapati hizo, mashuhuda hao walianza kumwaga sifa kibao  wakieleza kuwa kuna chapati ambazo wamekuwa wakipikiwa na Mama Lishe hao, ambazo hazina ubora na huenda hiyo inasababishwa na unga na mafuta yasiyo na ubora ambayo wamekuwa wakitumia.

 

Kila shindano kuna fitina zake; Theopista Cuthbert (mbele) wakati shindano likiendelea wajanja walimuibia jiko.

 

“Naam hizi ndiyo chapati, siyo zile nilizokula asubuhi pale kwa Mama Lishe,” alisema jamaa mmoja aliyeonja chapati za mmoja wa wapishi kwenye shindano hilo.

 

Mtangazaji wa Global Tv Online, Catherine Kahabi akimtangaza Esther Jonas (kushoto) kuwa mshindi wa kwanza.

 

Baada ya kukamilika kwa shindano hilo, mama lishe walioibuka washindi walizawadiwa khanga za Azania, mafuta ya Azania  (Azania Fresh)  na vifaa vya kupikia ili kuwawezesha kufanya kazi zao za mama lishe katika mazingira mazuri na safi.

 

Mama Babra a.k.a Mama Bonge, akitangazwa mshindi wa pili na kujizolea khanga, mafuta na unga wa ngano chapa Azania.

 

Unga wa Ngano wa Azania na mafuta ya kupikia ya Azania Fresh kwa sasa yanapatikana madukani kwa jumla na rejareja nchi nzima.

 

Mshindi wa kwanza, Esther Jonas, akikabidhiwa khanga ambapo pia alipewa mafuta na ngano.

Wikendi yako haiwezi kwenda poa kama hujapika chakula na mafuta ya Azania Fresh. Azania Group wanatumia teknolojia ya juu kabisa kuzalisha bidhaa zetu katika hali ya ubora na usafi.

 

Wateja wakionja chapati zilizokuwa zikishindaniwa.

 

Usikubali kuachwa nyuma. Matokeo ni mazuri kila wakati ukitumia unga wa ngano wa AZANIA wenye viwango kama vyote. Jaribu leo kutumia Unga wa Ngano wa Azania ujionee tofauti kwenye vitafunwa vyako, unga wa ngano wa uhakika.

 

Catherine akiwapa zawadi za ngano na mafuta ya Azania Fresh washiriki wa shindano hilo.

 

Kwa afya na Lishe Bora tumia leo Azania Fresh ujionee tofauti katika mapishi yako. Tumia AZANIA Fresh kwenye mapishi yako bila wasiwasi wowote kwa afya yako.

 

Jamaa wakijisevia chapati za Azania.

Wanarahisisha maisha yako kila siku kwa kuhakikisha wanakupatia bidhaa za uhakika na sasa wanakufikia popote ulipo. Piga wakufikishie bidhaa za uhakika kwa namba 0710 111 112 au tuma barua pepe kwa anuani ya email: [email protected]

PICHA ZOTE NA RICHARD BUKOS   

Leave A Reply