The House of Favourite Newspapers

Mama: Lulu Diva Alipenda Sana Kula Kuliko Kusoma

Mwanamuziki Lulu Abbas ‘Lulu Diva’.

IMEFICHUKA! Ndivyo unavyoweza kusema baada ya mama wa mwanamuziki Lulu Abbas ‘Lulu Diva’ kufunguka siri ambayo hajawahi kuisema popote, kwamba katika ukuaji wa mwanaye alikuwa anapenda sana kula kuliko shule.

 

Akizungumza na Ijumaa Wikienda , mama wa mrembo huyo alisema kipindi Lulu anasoma shule ya msingi alikuwa anapenda kum­fungia chakula ili aende nacho shule lakini matokeo yake alikuwa akifika shule anaanza kula kile chakula, kikiisha kabla ya masomo anarudi nyumbani bila kuingia darasani.

“Huyu Lulu alinisumbua sana, hu­wezi kuamini alikuwa anapenda kula kuliko masomo, nilikuwa nikimuan­dalia ‘paseli’ ya chakula kwa ajili ya kula ikifika mapumziko shuleni lakini cha kushangaza yeye alikuwa akila kabla na kikiisha anarudi nyumbani.

Stori: Na Memorise Richard

Comments are closed.