The House of Favourite Newspapers

Mama Mke wa Mtu Amwaga Radhi!

0

P1300198Stori: Dustan Shekidele, Ijumaa
Morogoro: Aibu! Mke wa mtu aliyefahamika kwa jina la mama Neema amejitoa fahamu na kumwaga radhi mbele ya umati wakiwemo watoto waliojitokeza kwenye sherehe ya kumtoa mtoto mwenzao iliyofanyika Mtaa wa Misufini Kata ya Chamwino mjini hapa mwishoni mwa wiki iliyopita.

Katika tukio hilo lililoshuhudiwa na gazeti hili, mama Neema alisaula nguo na kubaki na nguo nyepesi ya ndani huku ‘mazaga’ ya kiunoni yakionekana live.

Katika hali ya kushangaza na kuonesha kwamba mke huyo wa mtu aliamua dhahiri kumdhalilisha mumewe, alifanya uchafu huo mbele ya umati huo akiwemo mwanaye wa kumzaa, Neema aliyemshonea sare ya sherehe hiyo.

Kufuatia kitendo hicho, wanawake wenzake walioonesha kukerwa na kitendo hicho, waliamua kumfunika nguo lakini alibishana na kila mtu aliyejaribu kumzuia kufanya hivyo.

P1300202

Mama Neema akizidi kuonyesha ‘machejo’ yake.

Baada ya kuona hali hiyo, mwenye shughuli alimfuata DJ na kumuamuru kuzima muziki ambapo mama mwenye sherehe ya mwanaye, Asia Said ambaye ndiye aliyemualika shoga’ke huyo aliyeonekana kuzidiwa na ‘maji’, alimwita ndani na kumfungia hadi sherehe hiyo ilipokwisha.

Kwa mujibu wa watu wanaomfahamu mama Neema, siyo mara yake ya kwanza kumwanga radhi kwani alishafanya tukio lingine na kuacha watu midomo wazi.

“Huyu mama si mara ya kwanza kwani kuna siku alitembea utupu kwenye harusi iliyofanyika eneo la Kibao cha Shule, Chamwino ambapo wakati matarumbeta yakisindikiza maharusi, mama Neema alivua nguo zote na kuzishika mkononi, jambo hilo lilijaza umati uliojionea sinema ya bure,” alisema Fatuma Ally, mkazi wa Chamwino.

12027289_833678180080365_2770227947516259838_oBaada ya tukio hilo la kusaula mbele ya watoto, siku iliyofuata mwanahabari wetu alimpigia simu mama Neema na kumuuliza sababu za kumwaga lazi ilihali akijua ni mke wa mtu na mama wa watoto wawili ambapo alijibu:

“Wewe….(akitaja jina la mwandishi) kinachokukereketa ni nini? Umbeya tu umekujaa au umepagawa na mauno yangu?”

Leave A Reply