The House of Favourite Newspapers

Mama Mobeto Mwingine Ajitokeze!

0

BAADA ya madai kuzagaa kuwa siyo mama mzazi, mama wa mwanamitindo na msanii wa Bongo Fleva, Hamisa Mobeto, Shufaa Rutiginga, ameibuka na kusema, kama kuna mama mwingine wa mwanaye huyo, basi ajitokeze.

 

Mama Mobeto ameliambia Amani kuwa, anawashangaa wanaosema yeye siyo mama mzazi wa Mobeto, wakati hawajui hata robo ya chimbuko lake.

 

“Nashangazwa sana na habari hizi maana mtu anakomaa kwamba Misa (Mobeto) siyo mtoto wangu, sasa kama wanamjua mama mwingine, wamlete au ajitokeze maana hakuna mtu anayeweza kung’ang’ania mtoto wa mtu, watu waache maneno,” amesema mama Mobeto.

Stori: Imelda Mtema, Dar

Leave A Reply