The House of Favourite Newspapers

Mama Samia Aongoza Harambee Kuichangia Stars Dar – Video

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu  (katikati) akiwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto)  na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu  leo Juni 20, 2019 ameendesha harambee maalum ya kuichangia timu ya taifa (Taifa Stars) katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.

Timu hiyo inashiriki Fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON) zitakazofanyika Juni 21 hadi Julai 19 huko Misri.

 

Harambee hiyo ilizinduliwa rasmi Jumatatu iliyopita jijini Dar es Salaam na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na leo ndiyo kilele chake.

 

Katika hafla hiyo, Mama Samia amenunua jezi ya Taifa Stars kwa Sh. milioni  5.

 

Kampuni na taasisi mbalimbali za serikali na binafsi zimechangia kupitia kununua jezi, na  wadau kadhaa wamejitokeza kununua jezi hiyo.

Mamlaka ya Kudhibiti Mawasiiiano (TCRA)  wamenunua jezi za shl. millioni moja, Benki ya CRDB wamenunua jezi kwa sh. millioni moja, Kampuni ya mafuta ya  ORYX nao wamenunua jezi kwa sh. millioni moja,  na shirika la nyumba la taifa (NHC) wamenunua za sh. milioni moja.

 

Kampuni ya Kamaka – wamenunua jezi kwa milioni mbioli,  na Benki ya KCB imenunua jezi kwa milioni 1.5.

 

Mbali na Samia, viongozi wengine waliohudhuria ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe; Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda; Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Suzan Mlawi.

Comments are closed.