The House of Favourite Newspapers

MAMA: Sitaki Kuhusishwa na Wema

0

 

MZAZI anaposema hataki kuhusishwa na mambo ya mwanaye, Kibongobongo anakuwa anamaanisha nini; kwamba amemchoka au ametoa uhuru wa mtoto wake kujiamulia mwenyewe mambo yake?  Unajua kauli hii ya ‘sitaki kuhusishwa na mambo yake’ imetolewa na nani hivi karibuni? Imetoka mdomoni mwa Mariam Sepetu, mama mzazi wa Miss Tanzania 2006, Wema Isaac Sepetu ‘Madam.’

Sababu ya mama Wema kutoa kauli hiyo ni pale alipoulizwa na mwandishi wetu anaitazamaje hali ya kukongoroka mwili inayomkabili mtoto wake hivi sasa. ‘‘Sitaki kuzungumzia suala lolote linalomhusu Wema wala kitu chochote. Tayari ameshakua mtu mzima, ana maisha yake, mimi pia nina maisha yangu.

“Kwanza kwa nini mambo yake mniulize mimi? Sitaki kuongea chochote,” alisema mama Wema kwa sauti ya ukali. Mpaka mwandishi wetu anakata simu aliyotumia kuzungumza naye, hakuwa amejua ukali wa mama Wema ulimaanisha anafurahia hali ya kukonda aliyonayo mwanaye au ndiyo ameacha gari lifeli breki liende litakako?

Hivi karibuni mwili wa Wema, aliyekuwa ‘amefungasha’ siku za nyuma, umeonekana ‘kunyauka’ na kuwafanya baadhi ya watu kumuongelea kwa mitazamo tofauti. Kuna wengine wanasema anaumwa na baadhi wamehusisha kukonda kwake na utashi wa Miss Tanzania huyo kuamua kupunguza minyama uzembe kupitia dawa, mpangilio mzuri wa chakula na mazoezi.

 

Hivi karibuni Wema alinukuliwa na mtandao mmoja wa kijamii akisema anafurahia hali aliyonayo kwa sababu imemfanya kuwa mwepesi. Hata hivyo, mwonekano wake wa sasa umezidi kuleta gumzo hasa kwenye mitandao ya jamii kwa baadhi ya watu kusema ‘amependeza’ na wengine kudai amepoteza mvuto aliokuwa nao zamani.

Stori: Happyness Masunga, Amani

Leave A Reply