The House of Favourite Newspapers

Mambo mazito albam ya King Kiba

0

NI dhahiri kwamba Ali Saleh Kiba au King Kiba ni mfalme wa Bonge Fleva kwani ametoa albam ya Only One King iliyotoka Ijumaa ya wiki iliyopita.

Albam hiyo ni ya tatu kwa Kiba ina nyimbo 16 na yafuatayo mambo mazito ambayo unapaswa kuyajua kuhusu albam hiyo ambayo imepata mapokezi makubwa kwa mashabiki wa muziki ndani na nje ya nchi.

Uchunguzi umebaini kwamba, wasanii wa nchi tano ndiyo ambao wameshiriki kwenye albam hiyo; wasanii hao ni kutoka Tanzania, Kenya, Ghana, Afrika Kusini na Nigeria. Kenya ndiyo imetoa wasanii wengi kwenye albam hiyo.

Ndani ya albam hiyo zimetumika lugha tatu ambazo ni Kiswahili, Kingereza na Kifaransa. Kiswahili kimechukua zaidi ya asilimia 90, lakini jina la albam ni maneno ya Kingereza hivyo kuwa miongoni mwa albam za Kibongo zilizotoka bila kuwa na jina la Kiswahili.

Wasanii kutoka kwenye lebo yake ya King’s Music wameshirikishwa wao tu kwenye albam hiyo ambao ni Abdu Kiba, K2ga na Tommy Flavour.

Msanii wa Hip Hop pekee kutoka Kenya aliyeshirikishwa kwenye albam hiyo ni Khaligraph Jones ambaye ni Mshindi wa Tuzo ya African Music Magazine (AFRIMMA) mwaka 2018 katika Kipengele cha Msanii Bora wa Hip Hop Afrika.

Albam hiyo ya King Kiba imetoka chini na lebo mbili za King Music na Ziiki Media ambayo iliwahi kusimamia albam ya Darassa ya Slave Bocoming A King ambayo ilitoka mwaka 2020 ambayo pia Kiba alishirikishwa.

Albam hiyo, licha ya kuwa na nyimbo nyingi (16), lakini haijashirikisha mwanamke hata mmoja, tofauti na madansa na video queens.

Kwenye albam hiyo kuna makundi mawili yameshiriki ambayo ni Sauti Sol kutoka Kenya na Blaq Diamond kutoka bondeni Afrika Kusini.

Albam hiyo ya Kiba ni ya tatu kwa jamaa huyo ambapo ya kwanza ni Cinderella aliyoitoa mwaka 2007, ikafuata K4Real ilitoka mwaka 2009.

STORI; ELVAN STAMBULI, BONGO

Leave A Reply